Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DPP abadilisha hati ya mashtaka maafisa Polisi

Mshtakiwa, Majid Abdallah ( wa pili kutoka kushoto aliyejifunia kitamaa kichwani) akifuatiwa na Ramadhani Tarimo ( aliyevaa Sweta na kitambaa kichwani) ambao walikuwa Askari Polisi kabla ya kufukuzwa kazi,  wakiwa chini ya ulinzi wa Askari kanzu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa upya shtaka lao la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la unyang'anyi wa kutumia silaha na kuiba Sh90 milioni kutoka kwa Grace Donald Matage.

Dar es Salaam. Serikali imefanya mabadiliko katika hati ya mashtaka ya shitaka linalowakabili maofisa watatu wa Jeshi la Polisi kwa kuondoa namba zao za utambulisho wa ajira.

Maofisa hao wanakabiliwa na shtaka moja la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuiba Sh90 milioni, mali ya Grace Matage.

Kufuatia mabadiliko hayo, sasa hati mpya ya mashtaka itasomeka kama waliokuwa askari Polisi, baada ya kuvuliwa namba zao za utambulisho wa ajira na wamefukuzwa kazi na mwajiri wao, ambaye ni Jeshi la Polisi.

Wakili Serikali, Erick Kamala amewataja washtakiwa hao, kuwa ni Ramadhani Tarimo (42) maarufu kama Rasta na mkazi wa Kipawa;Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na Stela Mashaka, ambao wote walikuwa waajiriwa na jeshi la Polisi na  walikuwa askari kanzu wenye vyeo vya koplo.

Itakumbukwa kuwa Oktoba 31, 2023, washtakiwa hao walifikishwa mahakamai hapo na kusomewa shtaka moja la ungang’anyi wa kutumia silaha pamoja namba zao za utambulisho wa ajira kutoka jeshi hilo la Polisi.

Siku hiyo, washtakiwa hao walisomewa majina na mamba zao ambazo ni F 7149 D/ Coplo Ramadhani (42) maarufu kama Rasta; G. 7513 D/ Coplo Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na WP 6582 D/ Coplo Stela Mashaka.

Wakili Kamala, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Alhamsi Novemba 2, 2023, kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa kuondoa namba zao za ajira askari hao.

Kamala amedai mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, kuwa upande wa mashtaka unaomba kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka chini ya kifungu namba 234(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Wakili Kamala baada ya kueleza hayo, aliwasomewa upya shtaka lao, ikiwemo majina yao bila kutaja namba zao za ajira.

Akiwasomewa shtaka lao, wakili Kimala, alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namna 197/2023.

Alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo, Agosti 28, 2023 katika eneo la Kurasani, karibu na ofisi za Uhamiaji, lililopo wilaya ya Ilala, ambapo siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja waliiba Sh90 milioni kutoka kwa Grace Donald Matage.

Ameendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kabla na baada ya kufanya wizi huo, walimtishia Grace kwa bunduki ili waweze kujipatia fedha hizo bila kikwazo.

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalowakabili walikana.

Upande wa mashtaka wamedai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa shauri hilo, hivyo wanaiomba Mahakama hiyo, ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Msumi amewaambia washtakiwa hao, kuwa shtaka linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria hivyo, wataendelea kubaki rumande.

Baada ya kueleza hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.