Epukeni vishoka: Tanesco yaonya

Muktasari:
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Mhandisi wa Tanesco, Majige Mabulla amesema tangu Januari mwaka huu, hadi sasa kumeripotiwa majanga 18 ya moto, yaliyosababishwa na ‘vishoka’ kuunganisha umeme majumbani.
Dar es Salaam. Shirika la Umeme nchini(Tanesco) limesema majanga ya moto yanayotokea majumbani yansababishwa na uzembe wa wateja na Tanesco wasihukumiwe.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Mhandisi wa Tanesco, Majige Mabulla amesema tangu Januari mwaka huu, hadi sasa kumeripotiwa majanga 18 ya moto, yaliyosababishwa na ‘vishoka’ kuunganisha umeme majumbani.
Amesema matukio ya moto ni adimu kutokea endapo mfumo wa usukaji nyaya katika jengo unafanywa na wataalamu wenye ujuzi.
“Matumizi ya vitu kama pasi na mashine za kufulia na kuchemsha maji ndio chanzo cha moto majumbani hapo tatizo sio la shirika ni la wa tumiaji”amesema.
Amesema Tanesco hutoa fidia kwa wahanga wa majanga yaliyosababishwa na kuongezeka kwa umeme kuliko uwezo wa miundo mbinu ambapo kwa kawaida tatizo hilo huathiri nyumba zaidi ya moja zilizo katika mkondo huo .
“Tatizo la umeme kuzidi na kusababisha hitilafu haliunguzi nyumba moja bali mkondo wote uliounganishwa kwenye mfumo huo,” amesema