Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Exim, JKCI watia nguvu mapambano ya magonjwa ya moyo

Muktasari:

  • JKCI inasherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa kinara wa huduma za moyo Afrika Mashariki.

Dar es Salaam. Katika kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), benki ya Exim Tanzania imeshirikiana na taasisi hiyo kuendesha kampeni maalumu ya upimaji na elimu ya afya ya moyo kwa wafanyakazi wake, lengo likiwa ni kuhamasisha kinga na uchunguzi wa mapema wa magonjwa ya moyo.

Zoezi hilo lililofanyika katika Makao Makuu ya Exim Tower jijini Dar es Salaam, lilijumuisha vipimo vya shinikizo la damu, kipimo cha uzito na urefu (BMI), ushauri wa lishe na vipimo vya moyo (ECHO)

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Exim Bank, Stanley Kafu amesema ugonjwa wa moyo ni changamoto inayoongezeka na benki hiyo imeamua kuwekeza katika kinga, ikianzia kwa wafanyakazi wake.

“Afya ya moyo ni msingi wa ustawi wa mtu na taifa. Tumejipanga kuendelea kushirikiana na JKCI si tu kwa kampeni za ndani bali pia nje ya nchi, mfano kambi yetu ya pamoja ya matibabu Comoros mwaka 2024 iliyookoa maisha na kuonesha uwezo wa madaktari wetu,” amesema Kafu.

Kwa upande wake, Dk Tulizo Shem wa JKCI amesema uchunguzi wa mapema huongeza nafasi ya kuishi kwa wagonjwa wa moyo na kuokoa gharama za matibabu makubwa.

“Ushirikiano kama huu unaongeza uelewa na kupeleka huduma karibu na wananchi. Ndiyo njia bora ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza yanayoongezeka nchini,” amesema Dk Shem.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha magonjwa ya moyo ndiyo chanzo kinachoongoza cha vifo duniani, huku Tanzania ikikabiliwa na ongezeko la wagonjwa kutokana na mabadiliko ya maisha.

JKCI inasherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa kinara wa huduma za moyo Afrika Mashariki.