Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fisi aua mmoja, ajeruhi sita Tarime

Muktasari:

  • Mtu mmoja amefariki na wengine sita kujeruhiwa sehemu mbalimali ya miili yao baada ya kushambuliwa na fisi wilayani Tarime mkoa wa Mara

Musoma.  Mtu mmoja amefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na fisi katika mitaa ya mji wa Tarime mkoani Mara.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati watu hao waliposhambuliwa kwa nyakati tofauti walipokuwa wakielekea kwenye majukumu yao ikiwemo shambani.

Mkuu wa wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele amemtaja mtu aliyefariki baada ya kujeruhiwa kichwani na shingoni na fisi huyo kuwa ni Mang'ere Francis mkazi wa Tarime.

" Walijeruhiwa  sehemu tofauti tofauti ila watu wawili ndio walikuwa na hali mbaya kwani walikuwa na majeraha vichwani, midomoni na shingoni na madaktari walikuwa wanawaandaa hao watu wawili ili wakimbizwe hospitali ya rufaa ya mkoa lakini bahati mbaya mmoja akafariki dunia," amesema.

Amesema kuwa baada ya watu hao kushambuliwa kwa nyakati tofauti taarifa zilitufikia na hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha Keshi wilayani humo walianza kumsaka fisi huyo na kufanikiwa kumuua.

"Kwa kweli hadi sasa hatujajua huyu fisi alitokea wapi maana tukio limetokea mjini hata sio jirani na hifadhi na ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa majeruhi walifikishwa hospitalini.

“Nadhani yule mmoja aliyejeruhiwa sana atakuwa amefikishwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi baada ya mmoja kufariki," amesema.