Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Flatey: Sipigi tena sarakasi

Muktasari:

  • Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mkoani Manyara, Flatey Massay amesema hataruka tena sarakasi kwa kuwa Serikali imetenga fedha za ujenzi wa barabara aliyopigia kelele kwa muda mrefu.

Mbulu. Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mkoani Manyara, Flatey Massay ameishukuru Serikali kwa kutenga Sh8 bilioni za ujenzi wa barabara aliyoiombea fedha kwa zaidi ya miaka saba, hivyo hataruka tena sarakasi.

 Flatey ameyasema hayo wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 0.6 iliyopo kata ya Haydom.

Hivi karibuni akiwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bungeni jijini Dodoma, aliruka sarakasi kuonyesha hisia yake kwa barabara ya lami kutojengwa.

Hata hivyo, leo Juni 19 amesema hivi sasa hawezi kupiga tena sarakasi baada ya Serikali kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo eneo la Haydom.

"Sarakasi ya Bungeni imejibu kwani serikali imetenga sh8 bilioni za awali za ujenzi wa barabara ya kutoka Karatu kupitia Mbulu, Haydom hadi Sibiti," amesema Flatey.

Amesema amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka saba huku akiisemea barabara hiyo kwa muda huo na sasa imetengewa fedha ili ujenzi uanze.

Kiongozi wa mbio za mwenge Sahili Nyanzabara Geraruma amempongeza mbunge huyo kwa namna anavyowasemea wananchi wa eneo hilo.

"Wewe ni mkimbiza mwenge mwandamizi tunakuona kwenye vyombo vya habari namna unavyoisemea Mbulu na changamoto zake," amesema.

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mkoani Manyara, Flatey Massay akizungumza wakati mwenge wa uhuru ulipozindua barabara ya lami ya urefu wa kilomita 0.6 iliyopo Kata ya Haydom. Picha na Joseph Lyimo

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Abubakary Kuuli amesema ukiwa halmashauri ya Wilaya hiyo mwenge umetembelea miradi mitano ya thamani ya sh1.4 bilioni.

Kuuli ametaja miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, kiwanda cha chaki, kituo cha afya, ujenzi wa barabara ya lami na mradi wa maji.