Gari la kwanza la umeme lazinduliwa Tanzania

Muktasari:

  • Mchoraji katuni wa Tanzania, Masoud Kipanya amezindua rasmi gari lake ambalo ni la kwanza la umeme kutengenezwa hapa nchini.





Dar es Salaam. Mchoraji katuni wa Tanzania, Masoud Kipanya amezindua rasmi gari lake ambalo ni la kwanza la umeme kutengenezwa hapa nchini.

Kipanya, amesema gari hilo la umeme ni wazo lake binafsi la ubunifu ambalo lilimchukua miezi 11 kukamilika.

Gari hilo ambalo ni rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii nishati ya mafuta linaitwa Kaypee Motor na linachajiwa kwa saa sita kabla ya kutumika.

 "Hili ni gari la nguvu sana ambalo ukinunua unapata na chaji yake," alisema Kipanya wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Dar es Salaam Serena na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.