Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gesi asilia kuanza kusambazwa nchi nzima

Mtaalamu wa gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Eva Swila akiwasilisha mada katika warsha ya kuwajengea uwezo wanahabari mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Stephano Simbeye

Muktasari:

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema limeandaa mpango maalumu wa kuanza kusambaza nishati ya gesi asilia kupitia mabomba makubwa kwa lengo la kuwafikia wateja wengi katika mikoa mbalimbali nchini.


Mbeya. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema limeandaa mpango maalumu wa kuanza kusambaza nishati ya gesi asilia kupitia mabomba makubwa kwa lengo la kuwafikia wateja wengi katika mikoa mbalimbali nchini.

Mtaalamu wa idara ya mafuta na gesi kutoka TPDC, Mhandisi Eva Swilla amesema hayo leo Alhamisi Desemba 15, 2022 kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo 20 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwapo Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Ruvuma.

Mhandisi Swilla amebainisha hayo alipoulizwa kuwa ni lini TPDC litaanza kusambazwa gesi asilia kwa wananchi ili waweze kutumia nishati ya gesi badala ya kuni na mkaa.

Akijibu swali hilo Mhandisi Swilla amesema Serikali kwa kushirikiana na JAICA imeandaa mpango maalumu wa kusambaza gesi kupitia mabomba makubwa ambayo yatasafirisha kwa kiwango kikubwa na njiani yanasambazwa kwa mabomba madogo kuwafikia wateja.

Amesema mojawapo ya bomba hilo ni kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuwa hadi sasa kilometa 1,103 za mabomba yametandazwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es salaam.

Kuhusu uchafuzi wa mazingira Swila amesema watu wanachanganya kati ya gesi ya mitungi LPG, bali gesi asilia inayopatikana ardhini ni safi.

"Gesi ya mitungi inapatikana katika hatua ya kusafisha mafuta ambapo ni moja ya uchafu unapatikana katika hatua hiyo na kuwa inatoka nje ya nchi" amesema.

Amesema kiasi cha gesi asilia kilochogundulika kinatumika kinatumika kwa asilimia 70 katika kuzalisha umeme wa gridi ya Taifa, kuendesha mitambo katika viwanda 53, gesi imeingizwa katika nyumba 1,500 na kuanza kutumika katika magari 1,500.