Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GGML yaangazia mchango sekta binafsi maendeleo endelevu

Makamu wa Rais wa Uendelevu na Ushirikishwaji wa Wadau wa GGML, Simon Shayo.

Muktasari:

  • Kampuni hizo ni Geita Gold Mining Limited (GGML), ni miongoni mwa wadhamini wa Tuzo za Business SDG 2026 zitakazofanyika jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa, Juni 26, 2026.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayotambua sekta binafsi kama mhimili muhimu wa ukuaji wa uchumi, kampuni mbalimbali zimeendelea kuonesha mchango wao katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu nchini.

Miongoni mwa kampuni hizo ni Geita Gold Mining Limited (GGML), ambayo ni miongoni mwa wadhamini wa Tuzo za Business SDG  2026 zitakazofanyika jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa, Juni 26, 2026.

Tuzo hizo zinazoandaliwa na Global Compact Network Tanzania (GCNT) zinalenga kutambua kampuni na taasisi zinazotekeleza kwa vitendo Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kupitia shughuli zao za biashara na uwekezaji katika jamii.

Ushiriki wa GGML katika tukio hilo unaakisi nafasi ya sekta ya madini katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Kampuni hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake katika Mkoa wa Geita kwa zaidi ya miaka 25 na kwa sasa inaajiri zaidi ya watu 7,000, wengi wao wakiwa Watanzania.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, katika kipindi cha uendeshaji wake imechangia zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.7 kupitia kodi, tozo na michango mingine kwa Serikali, huku ikiendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya jamii inayozunguka maeneo yake ya shughuli.

Miradi hiyo inahusisha mafunzo kwa wahitimu wa vyuo, uhifadhi wa mazingira, huduma za afya, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na programu za maendeleo ya uchumi wa jamii.

Makamu wa Rais wa Uendelevu na Ushirikishwaji wa Wadau wa GGML, Simon Shayo, amesema sekta binafsi ina nafasi kubwa katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa, hususan katika kipindi ambacho Tanzania imejipangia dira mpya ya maendeleo ya muda mrefu.

Amesema majukwaa kama Business SDG Awards yanatoa fursa ya kuonesha na kutambua mchango wa kampuni mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za maendeleo kupitia uwekezaji wenye matokeo kwa jamii.

“Dira ya Tanzania 2050 imeweka matarajio makubwa kwa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya uchumi na ustawi wa wananchi. Hivyo ni muhimu kwa taasisi na kampuni kuendelea kuwekeza katika maeneo yanayogusa maisha ya watu na kuchangia maendeleo jumuishi,” amesema.

Shayo pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GCNT, taasisi inayoratibu shughuli za Umoja wa Mataifa zinazohamasisha biashara endelevu nchini.

Tuzo za Business SDG zimekuwa zikitumika kama jukwaa la kuhamasisha uwajibikaji wa kampuni katika shughuli zao za biashara pamoja na kutambua mchango wao kwenye kufanikisha maendeleo endelevu nchini.