Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakimu akwamisha kesi ya kuvujisha mitihani

Muktasari:

  • Katika kesi ya kusambaza mitihani ya Taifa ya darasa la saba kwa kutumia mtandao wa kijamii wa telegramu inayowakabili washtakiwa 12 wakiwemo walimu imeshindwa kuendelea kutokana hakimu anayeendesha shauri hilo kuwa na majukumu mengine.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza ushahidi katika kesi inayowakabili washtakiwa 12 wakiwemo walimu kwa kuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo anayeendesha shauri hilo yupo kwenye majukumu mengine ya kikazi.

 Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya kusambaza mitihani ya Taifa ya darasa la saba kwa kutumia mtandao wa kijamii wa telegram.

Wakili wa Serikali, Titus Haron aliieleza hayo leo Septemba 11, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji lakini Hakimu anayeendesha shauri hilo yupo kwenye majukumu mengine.

"Mheshimiwa naomba iahirishe hadi tarehe ya kesho Ili upande wa mashtaka tuweze kuendelea na ushahidi," amesema Haron.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 12, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji.

Washtakiwa hao  ni Jahnson Ondieka (37), Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nyanyakila , Gladius Roman, Lioyd Mpande, Ronald Odongo, Dorcas Muro,Alcheraus Malinzi, Jacob Adagio na Joel Ngome.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 2, 2022 na Oktoba 12, 2022 sehemu isiyojulikana washtakiwa hao walitengeneza nyaraka za uongo wa mitihani ya masomo ya Uraia na Maarifa ya Jamii ya darasa la saba wakijifanya mitihani hiyo ni halali na imeandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Pia tarehe hiyo na maeneo yasiyojulikana washtakiwa hao walivujisha mitihani ya Taifa ya darasa la saba kinyume cha sheria.