Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini yaporomoka

Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini yaporomoka

Muktasari:

  • Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa amesema ana wasiwasi na takwimu za kushuka kwa uhuru wa vyombo vya habari  kwa kuwa ni hali ya vyombo vya habari nchini sio mbaya.

Arusha. Hali ya  uhuru wa vyombo vya habari yashuka nafasi 53.

Akisoma hutuba ya taasisi za kihabari nchini, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile  amesema kwa majibu wa  taarifa ya waandishi wa habari wasio na mipaka dunia, tangu mwaka 2016 uhuru wa habari umekuwa ukishuka nchini.

Amesema mwaka 2016, kati ya nchi 180 Tanzania ilikuwa imeshika nafasi ya 71.

Balile amesema mwaka 2017, uhuru wa habari Tanzania ulishuka na  kufikia  nafasi ya 83 , mwaka 2018 ilishika nafasi ya 93 na mwaka 2020 imefikia namba 123.

"Anguko hili sio zuri tunaomba hali ya uhuru wa habari kuboresha nchini,"amesema Balile.

Amesema kutokana na hali hii ya uhuru wa vyombo vya habari,taasisi na wadau wa habari kuwa na mjadala wa kitaifa.

Hata hivyo, amesema wadau wa habari wanaimani kubwa na Serikali kutatua changamoto za wanahabari kama ambavyo imeanza kufanya.

Hata hivyo , Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa amesema ana wasiwasi na takwimu hizo kwa kuwa hali ya vyombo vya habari nchini sio mbaya.

Amesema Serikali inafanya kazi kubwa kuimarisha uhuru wa habari nchini.

Waziri Bashungwa amesema katika kuthibitisha hilo, hadi sasa Serikali imesajiri magazeti 246, runinga 53 na redio 194.

Waziri Bashungwa amesema jumla ya redio za mtandao 23 zimesajiriwa,blogs 120 na runinga za mtandaoni 440.