Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Halotel, Damu Salama kuchangisha chupa 500 za damu

Baadhi ya wanafunzi wa vyuoni mbalimballi wakichangia damu wakati wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Kampuni ya Halotel kwa kushirikiana na Kitengo cha Damu Salama mkoa wa Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Lengo ya kuke ni kuhakikisha kuwa mama mjamzito na mtoto hawapotezi maisha kwa kukosa damu.

Dar es Salaam. Katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu kwa wagonjwa wanaofikishwa katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati, kampuni ya Halotel Tanzania wakishirikiana na Kitengo cha Damu Salama, wamepanga kukusanya chupa 500 za damu kutoka kwa wanavyuo wa mkoa wa Dar es Salaam.

Chupa hizo za damu 500 zitakusanywa  katika kampeni ya uchangiaji damu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na na vyuo vya kati vya mkoa wa Dar es Salaam zoezi ambalo litaendeshwa na kampuni ya Mawasiliano ya Halotel.

Lengo ya kampeni hiyo ya uchangiaji damu ni kuwezesha mama mjamzito na watoto hawapotezi maisha kwa kukosa damu.

Akizungumza leo, Aprili 10, 2025 katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itakuwa haina kikomo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Biashara kutoka Halotel Abdallah Salum, amesema suala la kuokoa maisha ni jukumu lako, hivyo wanashirikiana na Kitengo cha Damu Salama kuokoa maisha ya jamii.

Hata hivyo, Salum ametoa wito kwa jamii kushiriki zoezi la kuchangia damu kusaidia kuokoa maisha ya wengine, hasa wagonjwa wa ajali, mama wajawazito, watoto wachanga, wagonjwa saratani na Ukimwi wanaohitaji damu mara kwa mara.

"Tunafanya kampeni hii katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu" amesema Salum.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Biashara kutoka Halotel, Abdallah Salum akizungumza wakati wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inashirikisha vyuo vikuu na vyuo vya kati vya mkoa wa Dar es Salaam.

Amebainisha kuwa kampuni hiyo kwa kushirikiana na kitengo cha damu salama mkoa itaendeleza dhamira yake ya kuwa karibu zaidi na jamii kwa kuhakikisha upatikanaji wa damu salama katika hospitali na vituo vya afya nchini, sambamba na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa uchangiaji damu wa mara kwa mara.

Kwa upande wake, Ofisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa  Damu salama kanda ya Mashariki, Joel Temba, alisema wameweza kushirikiana na kampuni ya halotel kwa ajili ya kuongeza chachu na hamasa juu ya ajenda ya uchangiaji wa damu nchini

"Wanafunzi wa vyuo na jamii wamejumuika hapa kuchangia damu, lengo likiwa ni kusaidia wakina mama wajawazito na watoto"

Amesema kwa jana pekee wamefanikiwa kukusanya chupa 104  za damu,lakini malengo yao ni kukusanya chupa 500 za damu.

Tumelenga vijana wa vyuo kwa sababu wanaweza kuwa  mabalozi wazuri na walimu wanapoenda kwenye jamii zetu na kwenda kutoa elimu ya uchangiaji damu kwa hiyari"

"Kila mtu anatakiwa atambue kwamba hatuna kiwanda cha damu, hakuna kisima cha damu, hivyo ni muhimu  kila familia kuwekeza akiba yake kwemye benki ya damu salama kwa ajili ya kesho"  Amesema.

Mery Lyimo ni mwakiishi kutoka kampuni ya  Woiso Original Products, anasema kampeni hiyo itasaidia kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma ya kuongezewa dawa.

Daktari bingwa kutoka Program ya Sikoseli( Selimundu) iliyochini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(Muhas), Dk Hilda Tutuba ameiomba jamii kuendelea kuchangia damu ilikusaidia wagonjwa hao kwani matibabu yake yanahitaji damu nyingi ili waweze kuokoa maisha yao.

" Ninawasihi jamii, wajenge tabia ya kujitolea kuchangia damu ili waweze kuokoa maisha ya jamii zetu" amesema Dk Tutuba.

Roxana Kadio ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, amesema kuwa kampeni yao imelenga pia kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na kuokoa maisha.

"Nashukuru hamasa imeenda vizuri kwani watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu hivyo wito wangu kwa jamii na vijana kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa elimu ili kuwekeza katika benki ya damu kwani hakuna kisima cha damu kinachoweza kusaidia wenye huitaji huo bali sisi tena kwa kujitolea,”amesema Kadio.

Razaki Hamza na Maria Abeid ni wanafunzi wa vyuo, ambao wamejitokeza katika kampeni ya kuchangia damu ili kuokoa maisha, ambapo wameipongeza kuwa kampeni hiyo.

" Suala hili ni la kuchangia damu ni suala linalogusa maisha ya watu na unapotoa damu kuokoa maisha ya watu wengine basi umefanya tendo kubwa la huruma kwa wenye uhitaji" amesema Maria

Kauli mbinu ya kampeni hiyo ni "Usalama wa mama na mtoto ni jukumu letu sote,Changia damu okoa maisha".