Hatima kesi ya Ole Nangole Jumatatu

Muktasari:

Hukumu hiyo inayosubiriwa kwa hamu mkoani hapa, inataraji kutolewa na jopo la majaji; Sauda Mjasiri, Profesa Ibrahim Juma na Musa Kipenka waliokuwa wanaisikiliza rufaa yake.  

Arusha. Hukumu ya rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumvua ubunge inatarajiwa kutolewa Jumatatu ijayo. Hukumu hiyo inayosubiriwa kwa hamu mkoani hapa, inataraji kutolewa na jopo la majaji; Sauda Mjasiri, Profesa Ibrahim Juma na Musa Kipenka waliokuwa wanaisikiliza rufaa yake. 

Wiki iliyopita, viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitinga mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa rufaa hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na makada wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Wakili wa Nangole, Method Kimomogoro amesema jana waliitikia wito wa Mahakama ambako walijulishwa kuwa hukumu hiyo itasomwa Oktoba 24 saa 11:00 asubuhi.