Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatua kwa hatua kamati ya Wafanyabiashara Kariakoo

Muktasari:

Kamati hiyo iliyojumuisha wajumbe 14 iliundwa baada ya mgomo wa siku tatu ya  wafanyabiashara uliolenga kushinikiza kuondolewa kwa kero zinazowakabili.

Dar es Salaam. Hatimaye Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa ajili ya kutatua mgogoro baina ya wafanyabiashara na Serikali, imemaliza kazi yake ya  kukusanya maoni na tayari imeikabidhi kwa Waziri Mkuu kwa hatua za awali.

Kamati hiyo yenye watu 14, iliundwa Mei 17, mwaka huu, baada ya kutokea kwa mgomo wa siku tatu wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo uliolenga kupaza sauti zao kutaka kutatuliwa kwa changamoto zinazokabili shughuli zao kubwa likiwa la utitiri wa kodi.

Katika hitimisho kati ya kikao cha wafanyabaiashara na Waziri Mkuu kilichofanyanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo, kuliundwa kamati hiyo kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuweza kushughulikia changamoto hizo.

Akizungumza leo Jumatano Juni 13, 2023 na Mwananchi Digital, Mwenyekiti Mwenza wa kamati hiyo, Hamis Luvembe, kuhusu hatua waliofikia hadi sasa, amesema wameshakamilisha kazi hiyo ikiwemo kuweka sawa maoni waliyopokea katika mtiririko mzuri na kutoa nao ya kwao pia.

“Baada ya kumaliza kazi hiyo, tumeshaikabidhi katika hatua za awali kwa Waziri aliyetupa kazi hii ili naye aipitie na wataalamu wake na kuona yapi yanaweza kutekelezeka na nina uhakika haitapita mwezi huu a tutakuwa tumeikabidhi rasmi hadharani kwa Waziri Mkuu,”amesema Luvembe.

Pamoja na hatua hiyo, mwenyekiti huyo aliwataka wafanyabiashara kuwa na subira katika kumalizia mchakato huo na kuwasihi kuendelea kulipa kodi bila shuruti.

“Wakati tukiwa katika mchakato wa kukusanya maoni kuna baadhi ya mambo yalipatiwa ufumbuzi wa haraka ikiwemo kukisitisha kikosi kazi cha ukusanyaji kodi.

“Lakini naomba wafanyabiashara hii isiwe sababu ya kuacha kulipa kodi kwa hiari wakati changamoto nyingine tukisubiri ifanyiwe kazi kupitia maoni tuliyoyakusanya kutoka kwenu,”amesema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara.

Akielezea changamoto walizokumbana nazo, alisema ni kuifanya kazi waliyopewa kwa  siku 17  badala ya 14 walizopewa awali na kubainisha kuwa hiyo imetokana na kukutana na changamoto ya usafiri katika kufika kwa wakati  katika mikoa mingine ikiwemo Kigoma na Bukoba walikotumia usafiri wa barabara baada ya kukosekana wa ndege.

Pia alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, ambako walitarajia wangetumia siku nne, walijikuta wakitumia siku tisa kutokana na wingi wafanyabiashara waliopo katika mkoa huo.

Kamati hiyo katika siku hizo 17 walifika mikoa 16 kukusanya maoni wakianza na Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye kujigawa makundi matano kwenda katika Kanda tano.

Kati ya hao wapo waliokwenda Zanzibar, Lindi na Mtwara, Kundi la pili lilikwenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Jingine lilikwenda katika mikoa ya Kigoma na Kagera na wengine Mwanza na Mara na lipo  lililokwenda Morogoro, Njombe, Mbeya na Songwe.