Hatua kwa hatua ya kuhifadhi taarifa zako kwa watumiaji wa iPhone

Hatua kwa hatua ya kuhifadhi taarifa zako kwa watumiaji wa iPhone

Muktasari:

  • Uwezekano wa simu kupotea, kuibwa au kuharibika upo wakati wote.

Uwezekano wa simu kupotea, kuibwa au kuharibika upo wakati wote. Huenda kitakachokuumiza zaidi baada ya simu yako kupotea ni kuzikosa taarifa zako muhimu kama vile namba za simu, picha au meseji.

Ni vyema kuhifadhi taarifa zako wakati wote ili utakapopoteza simu taarifa zako muhimu zibaki katika himaya yako.


iCloud vs. iTunes

Kuna namba mbili za kukuwezesha kuhifadhi taarifa zako nazo ni iCloud na iTunes. iCloud inahifadhi taarifa katika mtandao. Ni njia rahisi ya kuhifadhi taarifa.

Huhitaji kuhifadhi taarifa mpya kila siku isipokuwa simu yako inaweza kufanya yenyewe iwapo utaiamuru.

Mwisho wa uhifadhi taarifa hizo ni GB 5 na baada ya hapo utalazimika kulipia ziada.

iTunes itakuhifadhia taarifa zako katika kompyuta hata kama hutakuwa na mtandao.