Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hofu ya Juni 30 wahamiaji Afrika Kusini, Tanzania kuwarejesha raia wake

Muktasari:

  • Maelfu ya wahamiaji Afrika Kusini wanaendelea kukimbia nchi hiyo kuelekea Juni 30, huku hofu ya maandamano na mashambulizi ikizidi na serikali ikiongeza tahadhari ya kiusalama

Dar es Salaam. Hali ya taharuki imeendelea kutanda nchini Afrika Kusini huku maelfu ya wahamiaji wakianza kurejea katika nchi zao za asili kutokana na hofu ya kuongezeka kwa mashambulizi na maandamano ya kupinga wahamiaji yaliyopangwa kufanyika Juni 30.

Taarifa za vyombo vya habari nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa, wimbi hilo la wahamiaji kurejea katika nchi zao za asili limechochewa na kuongezeka kwa mikutano na maandamano yanayolenga raia wa kigeni, yaliyokuwa yakiratibiwa na baadhi ya makundi ya wananchi katika miezi ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa makundi hayo, Jumanne, Juni 30, 2026, ndiyo tarehe ya mwisho waliyoitaja kwa watu wanaodaiwa kuishi nchini Afrika Kusini bila vibali halali vya ukaazi kuondoka nchini humo.

Makundi hayo yameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya kile wanachodai kuwa ni ongezeko la uhamiaji haramu nchini humo.

Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo, serikali ipo katika hali ya tahadhari kuhakikisha usalama hasa ikizingatiwa kuwa makundi hayo yanapanga kufanya maandamano makubwa zaidi kesho Jumanne.

Serikali ya Afrika Kusini imesema inafuatilia kwa karibu mienendo ya makundi hayo ili kuzuia machafuko na kulinda usalama wa raia wote.

 Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesisitiza kuwa, serikali haitaruhusu watu kujichukulia sheria mkononi.

“Serikali pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia sheria za uhamiaji, vurugu na vitisho dhoidi ya raia wa ki8mataifa hazitakubalika,” amenukuliwa Rais Ramaphosa.

Hata hivyo, katika maeneo mbalimbali ya mijini, maelfu ya wahamiaji wameripotiwa kukusanyika katika makazi ya muda, karibu na ofisi za mabalozi wa nchi zao na maeneo yenye ulinzi, wakieleza hofu ya kiusalama.

Wahamiaji hao wanatajwa kuwa wengi wao wanatoka mataifa ya Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Ethiopia, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Baadhi ya nchi za Afrika tayari zimeanza kuwaondoa raia wao kwa ndege za dharura, huku zikieleza wasiwasi kuhusu usalama wa wananchi wao.

Kwa upande wake, Serikali ya Afrika Kusini imekanusha madai ya kushindwa kudhibiti hali hiyo, ikisema inachukua hatua zote kuhakikisha usalama wa watu wote bila kujali uraia wao.


Tanzania yachukua hatua

Tanzania ambayo wake wamo nchini humo, imeeleza mikakati inayoichukua kuhakikisha wanakuwa salama ama wanawarejesha nchini.

 Akizungumza na Mwananchi, leo Jumatatu Juni 29, 2026 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua zote za kiusalama kwa raia wa Tanzania waliopo huko akieleza kuwa, tayari imeratibu kuwasafirisha baadhi ya Watanzania kurudi nyumbani.

Amesema, juhudi za utambuzi wa vielelezo na kuwasaidia wasio na vielelezo hivyo kupata vibali kutoka mamlaka za nchi hiyo zimeshaanza huku wanawake na watoto wakipewa kipaumbele.

"Tatizo watu wetu baadhi hawana vielelezo, wengine wamekaa muda mrefu vimechakaa, hivyo tunaendelea kuwasaidia tangu juzi hapa Johannesburg na tutaendelea Pretoria. Tunazingatia zaidi wanawake na watoto katika hatua ya sasa," amesema.

Balozi Bwana amesema tayari orodha ya Watanzania 85 imeshawekwa kwenye ratiba ya kusafirishwa kupitia shirika la ndege Tanzania (ATCL) ambao utambuzi na vielelezo vikiwamo vibali, vitambulisho na hati za kusafiria akiweka wazi baada ya kukamilisha watasafirishwa kureheshwa nyumbani.


Chanzo cha mgogoro

Tishio kwa wahamiaji katika Taifa hilo limeibuka kutokana na kuongezeka kwa mikutano na maandamano ya makundi yanayopinga uhamiaji, ambayo yamekuwa yakidai ongezeko la wahamiaji wasio na vibali linachangia shinikizo la kiuchumi, ajira na kijamii.

Hali hiyo imezua hofu zaidi miongoni mwa wahamiaji na kuchochea wimbi la kuhama kabla ya Juni 30, baada ya siku hiyo kutajwa na waandamanaji kuwa mwisho kwa wahamiaji kuwepo nchini humo.

Baadhi ya wanasiasa, viongozi wa dini na mashirika ya haki za binadamu nchini humo wamekuwa wakilaani hatua hiyo kuwa inaweza kuathiri zaidi uhusiano wa taifa hilo na mataifa mengine.

Raia waliopo huko wakichangia mtandaoni wamepaza sauti zao kupitia mitando ya kijamii wakieleza hofu wanayopitia, wakisema hali ya amani ni tete kuelekea tarehe hiyo.

Neema Gaudence, amesema Watanzania wanaopata madhara ni wale wanaoishi sehemu za maisha ya chini ambako hakuna ulinzi imara akiomba Serikali kuwasaidia kurejea nyumbani.

"Kuna Watanzania wengi wanaishi Afrika Kusini maisha ya chini, vurugu zipo na zinaendelea kutuathiri," ameandika akiomba Serikali iwajali kwa kuwapatia msaada.

Killai Mipango ameiomba Serikali kuwarudisha nyumbani akisema hali ilivyo.

"Watu wenu tupo huku, ndio tupo kimakosa ila imeshatokea, nchi zote zinajali raia wao," ameandika kwenye ukurasa wa maoni kwenye taarifa ya Balozi, Bwana iliyorushwa na Clouds fm.

Milo Tae, ameandika kuwa wapo waliopoteza vitu vyao kutokana na ghasia hizo.

Naye Kigs Didaz amesema sehemu zenye makazi ya Wazungu ndizo zenye ulinzi akifichua kuwa maeneo ya raia wa kawaida kuna usumbufu.

"Mimi nipo Western Cape hapa Cape Town, hali siyo poa," ameandika.