Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hospitali ya Mkapa kuwezeshwa vifaa

Muktasari:

  • Rais John Magufuli alipohutubia mkutano maalumu wa CCM mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho, alisema ndani ya miaka minne iliyobaki katika uongozi wake atahakikisha kuwa Serikali inahamia Dodoma.

Dodoma.  Serikali imeanza kuangalia ni vifaa gani vya kupeleka  haraka katika hospitali ya kisasa, iliyopewa jina la  Benjamin Mkapa Utra Modern Hospital ili iweze kutoa huduma za afya zitakazoendana na idadi ya watu watakaohamia mjini hapa.

Rais John Magufuli alipohutubia mkutano maalumu wa CCM mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho, alisema ndani ya miaka minne iliyobaki katika uongozi wake atahakikisha kuwa Serikali inahamia Dodoma.

Hospitali hiyo ya kisasa iliyojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kuzinduliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ilianza kutoa huduma za matibabu mwishoni mwa mwaka jana.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Walemavu, Dk Khamis Kigwangalah amesema  Serikali kuhamia Dodoma kutasababisha ongezeko la wakazi katika mkoa huo kutoka 500,000 hadi milioni moja, kwa hiyo huduma za afya zinahitajika kuimarishwa.

Amesema kutokana na Dodoma kuwa katikati ya nchi, ni rahisi watu kutoka mikoa mingine kufika kupata huduma na kurejea mikoani kwao.

Mhandisi Upendo Busenya amesema toleo la mashine ya MRI iliyopo katika hospitali hiyo inapatikana nchi tatu tu duniani ambazo ni Tanzania, Afrika Kusini na Urusi.

Amesema mashine hiyo ni aina ya ‘Magnetom Spectra’ ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens yenye vipimo vinavyojulikana kwa kimombo ‘Magnetic field Strength 3 Tesla’ wakati  matoleo  yaliyopita ni 1.5 Tesla. “Inatoa picha zenye ubora wa hali ya juu kuliko matoleo yaliyopita,” alisema.

Kwa upande wa mashine ya CT Scan, Mhandisi Busenya amesema mashine waliyonayo inajulikana kama ‘Somatom flash’ yenye ubora kuliko matoleo yaliyopita baada ya kuboreshwa mambo mbalimbali.

Aliyataja mambo  yaliyoboreshwa kwenye toleo hilo ,kuwa ni muda wa kuchukua picha na kwamba ina uwezo wa kuchukua vipande vya picha 128 kwa mzunguko mmoja wakati matoleo mengine yalikuwa na uwezo wa kuchukua vipande vya picha 64 hadi 16. “Mzunguko mmoja unatumia sekunde 0.28 kumaliza nyuzi 360 na hutoa vipande vya picha 128,” alisema.