Hukumu kesi ya Sugu, Masonga inasomwa

Muktasari:
- Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite ameanza kusoma hukumu hiyo leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi.
Hukumu ya kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imeanza kusomwa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite ameanza kusoma hukumu hiyo leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi.
Kutokana na ulinzi kuimarishwa mahakamani, baadhi ya watu wamekusanyika vikundi vidogovidogo mbali na jengo la mahakama.
Katika eneo la mahakama wapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi nje ya jengo.
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.