Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya watu waliofariki katika ajali Momba, yaongezeka

Muktasari:

  • Ajali hiyo ambayo imesababisha vifo vya watu watano imehusisha malori mawili, bajaji na bodadoda

Tunduma. Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la Mpakani Wilaya ya Momba mkoani Songwe.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu leo Jumatano Juni 5, 2023; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Theopista Mallya amethibitisha kutokea ajali hiyo.

Kamanda Mallya amesema kuwa ajali hiyo imehusisha malori mawili, bajaji na bodaboda. "Ni kweli ajali imetokea imesababisha vifo vya watu watano na watu wengine 10 wamejeruhiwa, imehusisha lori moja la IT, bajaji, bodaboda na lori lingine ambalo limefeli breki."

Kamanda huyu amesema kuwa majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mpakani - Tunduma na taarifa kamili itatolewa baadaye.

"Imetokea majira ya saa sita mchana, bado tunafuatilia kujua chanzo cha ajali hiyo" amesema Kamanda huyo.