Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu

Muktasari:

  • Mfanyakazi wa shambani afungwa jela maisha gerezani baada ya kukiri kumbaka mtoto wa mwajiri wake mkoani Songwe.

Songwe: Mkazi wa Kitongoji cha Idodomya Wilaya ya Songwe Lucas Charles (35) ambaye ni mfanyakazi wa shambani amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kukiri kumbaka mtoto wa mwajiri wake mwenye umri wa miaka mitatu.

Akisoma hukumu hiyo leo Oktoba 26, Hakimu wa Wilaya ya Mbozi, Vitaris Changwe amesema kutokana na kuwa mshitakiwa amekiri kutenda kosa linalomkabili na kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho kimemwathiri mtoto katika maisha yake mahakama inamtia hatiani na kumhukumu kifungo cha maisha gerezani ili liwe fundisho kwa wengine.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka Pascal Manawe kuwa Oktoba 16 mwaka huu, katika Kitongoji cha Idodomya katika Kijiji cha Ngwara wilayani Songwe mshitakiwa alimchukua Mtoto huyo wa mwajiri wake na kwenda naye kusikojulikana na kisha baadaye kujulikana kuwa mtoto huyo amebakwa ndipo akipokamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi.

Manawe amedai kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na shitaka la kubaka chini ya kifungu cha 130, kifungu kidogo cha 1 na 2e na kifungu 131, kifungu kidogo 1 na 3 cha sheria na Kanuni ya adhabu sura 16 Kama kilivyofanyiwa marekebisho mwakata 2016.

Mshitakiwa huyo aliposomewa shitaka linalomkabili mahakamani hapo alikiri.

Aidha kwa upande wa mwendesha mashitaka aliomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na pia kuzingatia kuwa mshitakiwa alitenda kitendo hicho katika mazingira ya kuaminika kwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa mzazi wa mtoto.