Jela miaka 30 kwa kubaka mtoto

Asakwa na polisi akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka mitano, kumuua

What you need to know:

  • Mahakama ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imemtia hatiani, Yohana Lazaro (58) mkazi wa Kijiji cha Azimio Kata ya Matui kwa kosa la kubaka mtoto mdogo wa shule ya msingi.

Kiteto. Mahakama ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imemtia hatiani, Yohana Lazaro (58) mkazi wa Kijiji cha Azimio Kata ya Matui kwa kosa la kubaka mtoto mdogo wa shule ya msingi.

 Hatimaye kesi ya ubakaji namba 64.2022 iliyokuwa inamkabili Lazaro mkazi wa Kijiji Azimio Kata ya Matui wilayani Kiteto Mkoani Manyara, leo Aprili 24, 2023 imemalizika kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani kifungo cha miaka 30 jela.

Awali ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa kwa nyakati tofauti kuanzia machi na Desemba mwaka 2021 huko katika Kijiji cha Azimio, Kata ya Matui alimbaka mtoto huyo mdogo.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakama ya Wilaya ya Kiteto Juni 27, 2022 kwa kosa la ubakaji.

Baada ya kusomewa shitaka hilo mtuhumiwa alikana shitaka kisha hakimu wa mahakama hiyo Mosi Sasy kuamua kusikiliza pande zote mbili.

Akisoma shitaka hilo mahakamani hapo mwendesha mashataka wa Serikali, Joseph James alisema mtuhumiwa alitenda kosa kinyume na kif cha 130 (1) na (2) (e) na kifungu cha 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.

Hakimu Sasy baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote mbili alisema mahakama imesipitisha pasipo kuwa na shaka kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Joseph James mahakamani hapo alisema kuwa mtuhumiwa hana kumbukumbu ya makosa awali alimwomba hakimu Sasy kumpa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Mtuhumiwa alipotakiwa kuomba shufaa alisema hakuwa na cha kujitetea hivyo hakimu Mossi Sasy alimtia hatiani kifungo cha kwenda jela miaka 30.

Vitendo vya ubakaji Kiteto vimekithiri ambapo Mwananchi Digital limezungunza na na baadhi ya wananchi kupata maoni yao na kuomba wapimwe afya ya akili na sheria kali zichukuliwa kwa wanaobaka.

"Wanaobaka wapimwe afya akili..kwa hali ya kawaida mtu kubaka mtoto ni aibu na inafikirisha sana hivyo sheria ichukue mkondo wake," amesema.

Alisema vitendo hivi ni vya kujirudia mara kwa mara na mahakama imekuwa ikitoa adhabu kali akidai kwanini vinaendelea kujitokeza? anayekutwa na kadhia hiyo sasa apimwe afya ya akili amesema Mwita.

"Ni aibu sana kwa mwanaume mzee mtu mzima Kiteto kusikia amebaka mtoto wa chini ya miaka 10 anataka nini alichobakiza kwa mtoto huyo enzi ya ujana wake Serikali iendelee kuwachukulia hatua bila kujali jina umri wala kabila," amesema Hassani Mabwa mkazi wa Kibaya.