Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa kaka yake

 Rodick Msilwa akipanda gari la magereza baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 10. Picha na Mary Sanyiwa-Mufindi

Muktasari:

Katika utetezi wake,  mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama kuwa shauri hilo limeanzishwa dhidi yake kwa madai kwamba ni chuki, ugomvi kati yake na kaka yake huku chanzo kikiwa ni ugomvi wa ng'ombe.

Mufindi. Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Rodick Msilwa (20) baada  ya kumpata  na hatia ya  kumbaka mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka 10.

Hukumu ya kesi hiyo  namba 1,392 ya mwaka 2024 imetolewa jana Machi 13, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Benedict Nkomola.

Akisoma shtaka hilo, Hakimu Nkomola amesema tukio hilo limetokea Desemba 12, 2023 mchana huko Kijiji cha Luholofu, Kata ya Mgololo, baada ya mtoto huyo kutumwa shambani na mama yake kwenda kuchukua maharage,  lakini wakati anarudi ndipo alikutana na mshtakiwa na kubakwa.

"Alitumwa shambani na mama yake akiwa na mdogo wake wakiwa shambani waliitwa na mshtakiwa ambaye ni baba yake mdogo.Alimchukulia na kumpeleka kwenye nyasi kisha akamlaza chini na akamvua nguo yake ya ndani  akiwa amemziba mdomo ili asiweze kupiga kelele na  kumbaka na  baada ya kumaliza alimuahidi atampa Sh1,000 pamoja na pipi." ameeleza hakimu huyo.

Baada ya mshtakiwa kusomewa hati ya shtaka lake, alikana kutenda kosa hilo ndipo Mahakama ikaalika upande wa mashtaka kwa ajili ya kuthibitisha shtaka hilo.

Hakimu huyo amesema  upande wa mashtaka ulithibitisha shtaka hilo  bila kuacha shaka  kwa kuleta mashahidi sita pamoja na kielelezo kimoja cha  PF3 cha ofisa tabibu,  ambacho kilionyesha mtoto huyo aliingiliwa  sehemu zake za siri kwa sababu alikuwa na michubuko.

Aidha, baada ya kupitia ushahidi wa mashtaka Mahakama ilijiridhisha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu hivyo ni haki yake kujitetea kwa mujibu wa kifungu cha 231 cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Katika utetezi wake,  mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama kuwa shauri hilo limeanzishwa dhidi yake kwa madai kwamba ni chuki, ugomvi kati yake na kaka yake huku chanzo kikiwa ni ugomvi wa ng'ombe.

Hakimu baada ya kusikiliza utetezi huo akasema: " Kutokana na ushahidi ambao upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kosa bila kuacha shaka,  Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kumbaka lililopo katika kifungu 158(1) Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022 kwa kuzingatia kifungu cha 235 sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20 rejeo la  mwaka 2022.”

Hata hivyo, Hakimu amesema kwa kuzingatia sheria ya kifungu hicho 158(1) (a) cha sheria ya kanuni ya adhabu, mshtakiwa huyo amehukumiwa kutumia kifungo cha miaka 30 jela  huku akisema haki ya kukata rufaa imeelezwa.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,  Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Twide Mangula amesema kuwa upande wa mashtaka hawana kumbukumbu za nyuma dhidi ya mshtakiwa.