Jeshi la Russia kutumika kuokoa wanafunzi wa Tanzania Ukraine

Muktasari:

Russia imetengeneza njia ya usalama kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania walioko katika Chuo Kikuu cha Sumy (Sumy state university) ili  kuepuka mashambulizo ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine.


Dar es Salaam. Russia imetengeneza njia ya usalama kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania walioko katika Chuo Kikuu cha Sumy (Sumy state university) ili kuepuka mashambulizo ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini Russia leo Machi 5, 2022 kupitia mitandao ya kijamii, imewataka wanafunzi hao kuelekea eneo la Sudja ambako watapokelewa na jeshi la Russia.

“Kutoka Sudja watasafirishwa na jeshi hilo hadi eneo la Belgorod ambapo watapokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Moscow kwa taratibu zingine za kurejea nyumbani Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

Ubalozi huo pia umewashauri wanafunzi hao kutoka chuoni kwa makundi na kubeba bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha wanapopita kwenye safe corridor.

“Ili kurahisisha utaratibu wa mapokezi, wanahimizwa kuwasiliana na timu ya mapokezi wakifika eneo la Belgorod kupitia simu,” imesema taarifa hiyo ikitaja namba +79 267 666 228 WhatsApp +255 759 068 937.

Wanafunzi wa Kitanzania Ukraine waruhusiwa kuvuka mpaka wa Russia

Wanafunzi wa Kitanzania walio katika mji wa Sumy nchini Ukraine wameruhusiwa kutoka nchini humo kupitia mpaka wa Russia baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika na Serikali ya Russia kuridhia. Soma zaidi