JPM atoa msamaha kwa wafungwa 2,219

Rais John Magufuli

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Projest Rwegasira inaeleza kuwa wafungwa hao ni wale wenye magonjwa kama Ukimwi, saratani na Kifua Kikuu na wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70.

Dodoma. Rais John Magufuli leo ametoa msamaha kwa wafungwa 2,219 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Projest Rwegasira inaeleza kuwa wafungwa hao ni wale wenye magonjwa kama Ukimwi, saratani na Kifua Kikuu na wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70.

“Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” Imesema taarifa hiyo