Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jukwaa laundwa kuwaunganisha waandishi wa habari, watafiti

Mratibu wa taasisi ya InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo akizungumza jijini Mwanza kwenye warsha ya kutambulisha jukwaa la NileWell kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, watafiti na wadau wa mazingira

Muktasari:

Waandishi hao ni kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Ethiopia, Eritrea, Sudani Kusini, Sudan na Misiri.

Mwanza. Waandishi wa habari kutoka nchi 11 zinazohusiana na Mto Nile wataondokana na adha ya mlolongo mrefu wa upatikanaji wa tafiti na takwimu mbalimbali za kisayansi zinazohusu mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji.

Waandishi hao kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Ethiopia, Eritrea, Sudani Kusini, Sudan na Misiri wataondokana na adha hiyo baada ya kuunganishwa na wataalamu wa tafiti za hali ya mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji katika jukwaa la NileWell chini ya Taasisi ya Waandishi wa Habari ya InfoNile.

Akizungumza wakati wa warsha ya kutambulisha jukwaa hilo hivi karibuni kwa waandishi wa habari  nchini, Mratibu wa InforNile Tanzania, Said Sindo amesema jukwaa hilo litawapa fursa waandishi wa habari kuwasiliana moja kwa moja na watafiti lakini pia kuweka kazi zao.

“Jukwaa hili litakuwa chanzo muhimu cha upatikanaji wa tafiti na takwimu mbalimbali za kisayansi ambazo zitawasaidia waandishi wa habari katika uandishi wa habari za mazingira na Maji,”amesema

Mtafiti wa maswala ya mazingira na jiografia, Dk Laison Kaganga amesema jukwaa hilo litasadia kuzitambulisha tafiti zao haraka katika vyombo vya habari na kuwafanya watendaji kuwajibika ipasavyo katika maeneo yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi na viumbe hai.

Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut) ambaye pia ni Mtafiti, Ngogo Mang'enyi amesema awali kulikuwa na ushirikiano duni baina ya watafiti na waandishi wa habari hivyo jukwaa hilo limekuja wakati muafaka.

Mmoja wa waandishi wa habari walioshiriki katika warsha hiyo,  Sharifa Suleiman ambaye pia ni Katibu wa Jukwaa la Waandishi wa habari za maji na uhifadhi wa mazingira Tanzania (TAJOWEP) amesema watatumia jukwaa hilo ipasavyo kuhakikisha wanapata data mbalimbali.

Nyongeza na Nsekela Kasebele