Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UTPC mguu sawa kupambana na ukatili wa kijinsia

s

Morogoro. Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umeeleza kuwa unakusudia kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kwa sasa vimekuwa janga kwa Taifa.

Katika mapambano hayo UTPC imeanzisha kampeni maalum ya siku 16 ya kutoa elimu kwa jamii ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia  katika kundi la  wanawake na watoto hapa nchini.

Kampeni hiyo maalumu inayoshirikisha zaidi ya Waandishi wa habari 1,000 nchini imezinduliwa mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Keneth Simbaya amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto ni miongoni mwa ukiukwaji uliokithiri wa haki za binadamu .

 “Niwaeleze tukilifanya hili jambo kwa dhati litaleta mjadala mpana na hakuna mabadiliko yanayotokea kama watu hawajaelimika na vyombo vya habari haviwafundishi watu kufikiri lakini linawapa suala la kufikilia,”amesema Mkurugenzi huyo wa UTPC.

Mkurugenzi huyo pia amesema mabadiliko sahihi vyombo vya habari vitaangalia namna sheria zinafanya kazi na vitaweza kufanya uchambuzi na uchunguzi ili kuweza kubaini mapungufu yaliyopo ili kusaidia kuweza kupiga hatua.

“Kikubwa hatupendi kuona hatua zinachukuliwa baada ya tukio kutokea, tunalo jukumu kama waandishi wa habari kutoa elimu ili kuzuia matukio yasitokee watu wanasema kuzuia ni bora kuliko kuponya," amesema Simbaya.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa UTPC, Deo Nsokolo, Mjumbe wa Bodi hiyo, Lilian Kasenene amesema wanahabari wanalo jukumu la kuwa mstari wa mbele la kuwasemea wanawake na watoto ambalo ndio kundi kubwa linaloathirika na vitendo vya  ukatili wa kijinsia.

“Wapo wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia lakini kundi la wanawake na watoto ndio kundi kubwa zaidi linaloathirika na ukatili huo hivyo kama wanahabari wakipaza sauti zao itasaidia kupunguza vitendo hivyo," amesema Mjumbe huyo wa bodi.

Mwashabani Seif ambaye ni Mwandishi kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar, amesema Zanzibar kama sehemu ya Tanzania watahakikisha watapaza sauti kwa kushirikiana na UTPC ili kuondokana na janga hilo kwa kuwa waathirika ni watoto na wanawake .

“Watoto ndio Taifa la kesho hivyo wasipolindwa na kuwa matunda mazuri itakuwa ni janga kwa Taifa kwani humo humo ndio tunategemea kupata viongozi wakiwemo Marais, Mawaziri na viongozi wengine,”amesema  Mwashabani.

Kampeni hiyo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu inayoleza 'Wekeza, Zuia Ukatili wa Kijinsia'.

UTPC itatumia siku hizo 16 katika kutoa elimu ya kuandaa mada na mijadala mbalimbali ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, ukeketaji na vitendo vingine ambavyo vimekuwa na madhara makubwa na wakati mwingine hata kugharimu maisha ya watu.