Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi washirikiana na wanahabari kuwawezesha kutekeleza majukumu

Muktasari:

  • Polisi na wanahabari Songwe wakutana na kuondoa tofauti zao wasisitiza kila upande ufuate miongozo iliyopo.

Songwe. Jeshi la Polisi mkoani Songwe limewataka waandishi wa habari kuripoti mara moja wanapopata madhila wakati wanatimiza majukumu yao ili waliowafanyia hayo waweze kuchukuliwa hatua.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Oktoba 26 mwaka huu na mkuu wa Polisi jamii aliyemwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP Gallus Hyera wakati wa mdaharo wa majadiliano kuhusu madhila wanayopata waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao.

Amesema Jeshi la Polisi linasisitiza askari wake kuwa na nidhamu, kufanya kazi kwa weledi na haki lakini hapa na pale askari mmoja mmoja anakengeuka na kufanya kinyume na maelekezo hayo.

"Akikosea askari mmoja isihesabike kuwa askari wote ndivyo walivyo bali nyie wanahabari mkipata tatizo lolote kuhusu askari toeni taarifa kwa viongozi wao Ili hatua zichukuliwe mapema," amesema Hyera.

Aidha, amewasihi waandishi wa habari kujikita katika kujielimisha kitaaluma Ili wawe wabobezi na kuweza kufanya kazi yao kwa weledi.

Awali, akiwasilisha taarifa ya madhila kwa waandishi wa habari Ofisa Programu Msaidizi kutoka Umoja wa Vilabu Tanzania (UTPC), Edmund Kipingu amesema katika kipindi cha miaka 10 iliyopita tangu matukio ya madhila kwa wanahabari yalipoanza kurekodiwa jumla ya waandishi wa habari 272 wamepata madhila mbalimbali na mengi kati ya hayo yamefanywa na polisi.

"Madhila yaliyowapata waandishi wa habari ni pamoja na kukamatwa wakiwa kazini matukio 52, vitisho matukio 50, shambulio la mwili matukio 25, kufungiwa vyombo vya habari 29, faini 14, kuondolewa eneo la kazi matukio 10 kutekwa matukio 13 na matukio 15 ya kujaribiwa vifaa vya kazi," amesema Kipingu.

Kuhusu Mkoa wa Songwe, Kipungu amesema katika kipindi cha miaka 6 tangu mkoa kuanzishwa Kuna matukio 13 ambayo yametokea ambapo Jeshi la Polisi matukio 5, halmashauri za wilaya matukio 4, vyama vya siasa matukio 2 na mamlaka ya mawasiliano matukio 2.

Akitoa ushuhuda wake mmoja wa waandishi wa habari Jamal Meena amesema katika kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2020 Polisi walimkamata na kumpatia adhabu na kisha kumwamuru aache pikipiki yake kisha aende zake.