Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera wananchi wanakabiliwa Migogoro ya ardhi, kesi 200 kupokelewa kila mwezi kwenye mabaraza

Kaimu Katibu tawala Mkoa Kagera, Isaya Tendega akizungumzia changamoto ya migogoro na kesi katika semina na mafunzo iliyotolewa na waratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa watoa msaada wa kisheria katika halmashauri nane.

Muktasari:

  • Migogoro ya ardhi ni moja ya changamoto kubwa iliyotajwa kupokelewa kwa wingi katika mabaraza manne ya ardhi huku migogoro mingine kama ya mirathi pamoja na ukatili wa kijinsia ikitajwa kupokelewa katika mahakamani na vituo vya polisi kwa wingi.

Bukoba. Wananchi Mkoa wa Kagera wametajwa kukabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi, Mirathi na ukatili wa kijinsia huku ile ya ardhi ikihusishwa kupokelewa kwa wingi katika mabaraza.

Kaimu katibu Tawala Mkoa Kagera, Isaya Tendega akizungumza  na mwananchi Digital, leo Jumapili, Aprili 13, 2025 kwenye mafunzo ya watoa msaada wa kisheria halmashauri zote nane za mkoa yaliyoandaliwa na waratibu wa kitaifa wa Kampeni ya Mama Samia kutoka wizara ya sheria na katiba  inayotarajiwa kuzinduliwa mkoani Kagera Aprili 14 hadi 24, 2025 na waziri wa katiba na sheria.

Tendega, amesema kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imekuja muda mzuri kwa sababu itasaidia kutatua migogoro na kesi mbali mbali ikiwemo ile ya ardhi ambayo imegeuka tishio kwenye jamii ndani ya Mkoa wa Kagera.

"Kila siku ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia kitengo cha Sheria na utatuzi tunapokea migogoro na kesi nyingi zinazohusu ardhi, mirathi pamoja na ukatili wa kijinsia siwezi kutaja takwimu kila eneo ila changamoto ni kubwa inayohitaji msaada wa kisheria"

"Kesi nyingi na migogoro hapa tunashukuru sana na tunampongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuleta kitu hiki muda mwafaka tunaimani migogoro itapungua na kuisha"amesema Tendega

Amesema Kampeni hiyo kupitia wizara ya sheria na katiba itasaidia kuhakikisha wanatatua changamoto ya migogoro hiyo kwa wakati ili iweze kupungua katika mkoa huo.

Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika ukumbi kwa ajili ya kupata mafunzo hayo ya msaada wa kisheria kabla ya Kampeni hiyo inayotaratajiwa kuanza mkoa Kagera,14 Aprili, 2025.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Mkoa Kagera, Jovini Rutahinulwa amesema mkoa una wastani wa  mabaraza ya ardhi manne anbapo kila mwezi wanapokea changamoto ya kesi za migogoro ya ardhi 200 kwa maana ya mashauri ya msingi na yale ya maombi maalumu madogo.

Ameongeza kuwa ukiangalia hali hiyo unaona kuwa kuna changamoto kubwa ndomaana wanapokea kesi nyingi.

"Kampeni hii itasaidia kuelimisha jamii kuhusu maswala mbali mbali yanayohusu ardhi na kupunguza migogoro"Amesema Jovin

Mkazi wa manispaa ya Bukoba mkoa Kagera, Eliud Kwelebela amesema anatamani kuona Kampeni hiyo ikijita hasa maeneo ya vijijini maana hawana elimu jinsi ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili hasa za migogoro ya Ndoa Mirathi na ardhi.

"Elimu hawana wananchi wanaogopa ata kufika mahakamani au mabaraza ya ardhi inauma sana tunaomba msaada na hii kampeni izidi kuwepo licha ya viongozi kuizindua itapendeza ata ngazi za chini iendelee"amesema Eliudi

Hata hivyo,awali mkurugenzi wa Kampeni hiyo kitaifa (MSCLAC), Ester Msambazi ametangulia kusema kuwa mpaka sasa kupitia Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia wamefanikiwa kutoa elimu kwenye mikoa 24 na mkoa huo wa Kagera  unakuwa wa 25 huku akidai kuwa  elimu hio wamefikia zaidi ya asilimia zaidi ya 75 kwenye mikoa yote.

"Kufikia mwezi Mei, 2025 sisi kama wizara tunatarajia kuwa tumekamilisha Kampeni hii kwenye mikoa 26.

Msambazi, ameongezakwa kusema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha migogoro na mashauri mbali mbali  kwenye jamiii inatokomezwa kila kona ya Nchi.