Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera yaandikisha wanafunzi 60,743 wa darasa la kwanza

Ofisa elimu mkoa wa Kagera mwalimu Khalifa Shemahonge akiongea na Mwananchi digital kuhusu uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Kwa mwaka 2023 ambapo uandikishaji huo ulikoma Desemba 31,2022 richa ya kwamba hawa watakaokuja wamechelewa watapokelewa.

Muktasari:

  • Ofisa elimu mkoa wa Kagera, Khalifa Shemahonge amesema malengo ya uandikishaji kwa darasa la kwanza yalikuwa ni wanafunzi 86,348, wavulana wakiwa 42,645 na wasichana 43,703. Hadi Desemba 20, 2022 walikuwa wameandikishwa wanafunzi 60,743 sawa na asilimia 70,  wavulana 30,099 na wasichana 30,544.

Bukoba. Takribani wanafunzi 60,743, sawa na asilimia 70 wameandikishwa kuanza darasa la kwanza mkoani Kagera huku wanafunzi waliokwisha andikishwa kuanza darasa la awali wakiwa ni 50,404 sawa na asilimia 59.

 Ofisa elimu mkoa wa Kagera, Khalifa Shemahonge akiongea na Mwananchi leo Januari 02, 2023  amesema idadi hiyo ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza na awali inaishia Desemba 20, 2022 na ukomo wa kuandikisha wanafunzi hao ilikuwa Desemba 31, 2022.

“Maoteo kwa darasa la kwanza walikuwa ni wanafunzi 86,348, wavulana wakiwa 42,645 na wasichana 43,703. Hadi Desemba 20, 2022 walikuwa wameandikishwa wanafunzi 60,743 sawa na asilimia 70,  wavulana 30,099 na wasichana 30,544,” amesema Shemahonge.

Amesema maoteo ya wanafunzi wa awali yalikuwa ni kuandikisha wanafunzi 86,905 wavulana 42,898 na wasichana 44,007. Hadi Desemba 20, 2022 walikuwa wameandikishwa wanafunzi wa awali 50,404 sawa na asilimia 59 na kuwa uandikishaji wa awali na la kwanza ulikuwa unakoma Desemba 31, 2022.

“Lengo ni wanafunzi wote wakianza kusoma waanze siku moja ili isije ikafika mahali wanafunzi wengine wanaachwa nyuma kimasomo, changamoto ibaki kwa wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu wanafunzi wanaoingia la pili,” amesema.

Shemahonge ameongeza: “Miaka ya nyuma uandikishaji kama huu msingi na sekondari ulikuwa unakoma Machi 31, mwanafunzi ameanza Machi 31 wenzake walioanza Januari wanakuwa wamejifunza, hapo mwalimu analazimika kurudi nyuma ili awafundishe hawa walioanza wamechelewa. Lakini serikali iliona iondoe tatizo hilo la uandikishaji uishie Desemba 31 ya kila mwaka.”

Amesema hawatawafukuza watakaoandikishwa baada ya hapo lakini akasema wazazi wajue watoto wao watapata hasara kwani watakaowahi watakuwa wanaendelea kujifunza na kuwa wanaoanza darasa la kwanza ni kuanzia miaka sita hadi saba na awali ni kuanzia miaka minne hadi mitano.

Mmoja wa wazazi aliyeenda kuandikisha mwanafunzi wa awali, Ajuna Abdul amesema baada ya kumpekeka mtoto kumwandikisha darasa la awali katika shule ya msingi Rumanyika, ameambiwa alipe fedha ya mlinzi Sh4,000 na fedha ya uji Sh10,000 lakini Kwa kuwa alikuwa hana fedha, amelazimika kumrudisha mwanae nyumbani ili atafute fedha.