Karua apiga kura Giguchu, mashine zamgomea

Muktasari:

  • Mgombea mwenza wa Azimio La Umoja, Martha Karua amefanikiwa kupiga kura leo saa 12.10 asubuhi kwenye kituo cha uchaguzi cha Shule ya msingi Mugumo kwenye jimbo la Giguchu.


Nairobi. Mgombea mwenza wa Azimio La Umoja, Martha Karua amefanikiwa kupiga kura leo saa 12.10 asubuhi kwenye kituo cha uchaguzi cha Shule ya msingi Mugumo kwenye jimbo la Giguchu.

Karua aliwasili kituoni hapo saa 12 kamili asubuhi huku jina lake likigoma kusoma kwenye mfumo wa kieletroniki wa kupiga kura (KIEMS) kabla ya jitihada kufanyika na baadae kukubali.

Mgombea mwenza huyo amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa miaka mitano ijayo.

"Leo ni siku yetu hakikisha unaenda kupiga kura. Ninahisi kujiamini na ninajisikia vizuri siku ya leo,” amesema.