Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katuni kupinga unyanyapaa wa usonji yazinduliwa

Balozi wa Australia nchini Kenya, Luke Williams akizungumza katika uzinduzi wa katuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. 

Muktasari:

  • Shirika la Tai Tanzania limetengeneza katuni iitwayo Fidi kwa kushirikiana na kituo cha kutibu Watoto cha Gabriella Rehabilitation Centre kwa kutumia uzoefu wa watu hai wenye ugonjwa usonji Pamoja na familia zao na marafiki.


Dar es Salaam. Ubalozi wa Australia ukishirikana na shirika la Tai Tanzania wamezindua katuni mpya yenye lengo la kukuza ufahamu juu ya ugonjwa wa Usonji nchini Tanzania.

Katuni hiyo iliyopewa jina la Fidi inaeleza hadithi ya mvulana mwenye usonji, ikionyesha maisha yake ya kila siku, changamoto anazozipitia na namna anavyozikabili.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtoto mmoja miongoni mwa watoto 100 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa usonji na inakadiriwa kuwa asilimia 1.2 ya Watanzania wamegundulika kusumbuliwa na ugonjwa huo.

Wagonjwa hao pia wanakabiliwa na unyanyasaji na unyanyapaa unaowaathiri na kuwakatisha tamaa wengine wanaotaka kupima.

Kutokana na kadhia hiyo, sirika lisilo la faida la Tai Tanzania limeandaa hadithi kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kijamii na kitabia kwa kutumia katuni za mtindo wa 3D, maigizo ya redio na vijarida vya katuni.

Akizungumza leo Novemba 8 katika uzinduzi huo Balozi wa Australia nchini Kenya, Luke Williams amesema watu wote wakiwemo wenye usonji wana haki ya kufurahia afya ya mwili na akili.

“Bado Watoto wenye usonji wamekuwa wakikumbwa na unyanyapaa na unyanyasaji nchini Tanzania na ulimwenguni kote.

“Katuni hii ni hatua bora ya kutoa elimu kuhusiana na usonji miongoni mwa vijana na jamii kwa ujumla,” amesema.

Amesema machapisho yenye katuni hiyo yatatumika kufikisha jumbe muhimu kwa jamii, hususani vijana wa rika dogo nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Programu na Uendeshaji, Debora Maboya amesema hadi leo zaidi ya wanafunzi 2,000 katika shule saba jijini Dar es Salaam wamekwisha tazama katuni hiyoo.

“Wamefanya majadiliano na kutoa mitazamo yao. Tunategemea kusambaza katuni hii zaidi nchini Tanzania na kwenye mitandao katika miezi ijayo,” amesema.