Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi achangisha Sh100 milioni kusaidia wenye usonji

Muktasari:

  • Fedha hizo zilikabidhiwa kwa mfano wa hundi Januari 19, kwa taasisi ya Lukiza Autism ambao watatekeleza mradi wa mwaka mmoja kwa wanafunzi wa Msimbazi Mseto Jijini Dar es Salaam, kiwa ni pamoja na mazoezi tiba.

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Madeline Kimario amechangisha Sh100 milioni kwa ajili kuwasaidia wanafunzi wa shule ya msingi ya Msimbazi Mseto wenye changamoto ya usonji.
Fedha hizo zilikabidhiwa kwa mfano wa hundi Januari 19, kwa taasisi ya Lukiza Autism ambao watatekeleza mradi wa mwaka mmoja kwa wanafunzi wa Msimbazi Mseto Jijini Dar es Salaam, kiwa ni pamoja na mazoezi tiba.
"Kama sehemu ya masomo yangu nilikuja na wazo la kusaidia wanafunzi wenye changamoto hii na jambo la kwanza lilikuwa ni kuandika pendekezo nililopeleka kwa watu binafsi, vikundi na taasisi tofauti kwa msaada wa shule yangu.
"Fedha iliyopatikana kuanzia Septemba mwaka 2022 niliamua kushirikiana na Lukiza nikijua kwamba wanaweza kutumia mchango huo kwa wale wanaohitaji," amesema Kimario.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism, Hilda Nkabe amesema wao sehemu ya mradi wao fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kutoa tiba kwa mwaka mzima kwa wanafunzi wasiopungua 15, kutoa usafiri wa kwenda na kurudi shuleni.
Nkabe amesema fedha hizo zitatumika pia kukarabati vyumba vya tiba, na kutoa vifaa kwa ajili ya matibabu. matibabu.
"Kampeni ya uelewa wa Usonji na kusaidia matibabu ya afua ni malengo mawili ya Lukiza Autism Foundation katika mpango wake wa kimkakati. Hii inafungamana kikamilifu na mradi wa Madeleine wa kurudisha kwa mchango kwa jamii," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Afyacheckers Consultants, Dk Romana Malikusema atakayewezesha kutoa tiba kwa wanafunzi hao amesema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo kuwajengea uwezo walimu wenye mahitaji maalum waliopo Msimbazi Mseto Autism.
Naye Ofisa Elimu Mahitaji Maalumu Jijini Dar es Salaam, Swalehe Msechu alitoa shukurani zake kwa niaba ya Kituo cha Autism cha Msimbazi Mseto kwa Madeleine na Lukiza kwa kuchangisha fedha hizo na kuchagua kukisaidia kituo hicho.
Mwalimu Mkuu wa Msimbazi Mseto, Joyce Sanka alisema kwa hatua hiyo changamoto kubwa ya usafiri kutoka nyumbani hadi shule kwa wanafunzi hao inakwenda kutatuliwa lakini pia itasaidia upatikanaji wa chakula kwa watoto.
"Tunatumaini wadau wengine watajitokeza kuwasaidia watoto hawa ili wote wasome katika mazingira rafiki na wawe na uhakika wa kuja na kurudi nyumbani," amesema.