Kauli ya Diamond baada ya kukosa tuzo BET

Kauli ya Diamond baada ya kukosa tuzo BET

Muktasari:

Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono licha ya kushindwa kunyakua tuzo ya ‘Best International Act’ ya BET iliyokwenda kwa msanii wa Nigeria, Burna Boy.

Dar es Salaam. Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono licha ya kushindwa kunyakua tuzo ya ‘Best International Act’ ya BET iliyokwenda kwa msanii wa Nigeria, Burna Boy.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram leo Jumatatu Juni 28, 2021, Diamond amesema, “kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani Watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu. Nawashukuru sana kila mmoja wenu kwa upendo mkubwa mlionionesha ni faraja kuona dunia inapotaja nchi zenye wanamuziki bora Tanzania inatajwa, ni jambo la kumshukuru Mungu, naamini wakati mwingine tutaibeba.”

 "Nitafarijika kesho na kesho kutwa msanii mwingine pia akiwa katika jambo la kuwakilisha Taifa tumpe nguvu kama mlionipa, sisi ni SwahiliNation sisi ni Taifa la Waswahili," amesema.

Katika tuzo hizo Diamond alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki.