Kesi ya akina Mbowe kuendelea, shahidi wa tano akitoa ushahidi

Tuesday November 02 2021
KESI 1 PIC
By James Magai
By Fortune Francis

Dar es Salaam. Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi, leo tena inatarajiwa kuendelea kuunguruma katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Mahakama hiyo leo inatarajiwa kuendelea kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka kutoka kwa shahidi wa tano.

SOMA: Mwanzo mwisho shahidi wa nne kesi ya kina Mbowe

Tayari washtakiwa wameshafikishwa mahakamani na wako mahabusu wakisubiri muda wa kupandishwa kizimbani.

Mawakili wa pande zote pia wameshafika mahakamani. Mawakili wa utetezi wengi wako tayari wameshaingia katika ukumbi wa mahakama na kukaa kwenye nafasi zao huku mawakili wa Serikali wakiwa bado ofisini kwao hapa mahakamani, wakiendelea na maandalizi, wakimwandaa shahidi wao kabla ya kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.

Mpaka sasa ni Jaji Joachim Tiganga ndio anayesubiriwa.

Advertisement

Tutaendelea kukuletea mwenendo wa kesi hii moja kwa moja kutoka mahakamani kadri itakavyokuwa ikiendelea.

Advertisement