Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya anayedaiwa kumtapeli mstaafu Sh315 milioni yaiva

Watu saba wafikishwa kortini wakidaiwa kujipatia Sh 428milioni mali ya Tanesco

Muktasari:

  • Prepetua anadaiwa kumtapeli mstaafu kiasi hicho cha fedha kwa madai kuwa anataka kufanya biashara, wakati akijua ni uongo.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, imepanga Septemba 7, 2022 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kujipatia Sh 315milioni kwa njia ya udanganyifu, inayomkabili Prepetua Gondwe (28) maarufu kama Annastazia.

Hiyo ni baada ya upelelezi wa shauri hilo la jinai namba 114/2022, kukamilika.

Prepetua ambaye ni mkazi wa Kigamboni, anayedaiwa kumtapeli mstaafu kiasi hicho cha fedha, kwa madai kuwa anataka kufanya biashara, wakati akijua ni uongo.

Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava, ameieleza mahakama hiyo, leo Agost 29, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kumsomewa mshtakiwa hoja za awali (PH).

Mshtakiwa baada ya kusomewa maelezo yake, amekana hoja tano na kukiri hoja moja.

Hoja alizokana mshtakiwa huyo ni kwamba hahusiki na mashtaka mawili yaliyopo mahakamani hapo, amekana kukamatwa na kufikishwa kituoni, pia amekana kuhojiwa Polisi,

Vile vile amekanakuwa hakuwahi kukiri kujipatia fedha hizo akiwa kituo cha Polisi na wala hajui kama nyaraka mbalimbali ikiwemo simu yake ya mkononi, vilichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi.

Hoja alizokubali mshtakiwa ni majina yake na siku akipofikishwa mahakamani.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 7, 2022 itakapoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi.


Mshtakiwa huyo ambaye ana mtoto mdogo, amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Itakumbukwa Agosti 18, 2022, Prepetua alifutiwa kesi ya jinai yenye mashtaka kama hayo na kisha kufunguliwa kesi nyingine, ambayo ndio hiyo ipo mahakamani kwa sasa.

Sababu ya kuifuta kesi hiyo na kufunguliwa nyingine inatoka na mshtakiwa huyo kuiomba Mahakama hiyo urudie kusikiliza ushahidi kuanzia shahidi wa watatu hadi wa sita wa upande wa mashtaka ambao tayari walishatoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa.

Inadaiwa kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya zamani, mshtakiwa huyo aliruka dhamana, hali iliyopelekea kesi hiyo kuendelea bila kuwepo mshtakiwa mahakamani.

Siku hiyo mshtakiwa alidia kuwa wakati wa usikilizwaji wa mashahidi hao yeye hakuwepo hivyo hajua anatuhumiwa kwa makosa gani.


Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, aliyekuwa anasikikiza shauri hilo, Huruma Shaidi alimueleza mshtakiwa kuwa aliruka dhamana na kushindwa kuhudhuria kesi yake hadi alipokamatwa na kupelekwa mahakamani.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Shaidi alisema ili mshtakwa aweze kupata nafasi ya kusikiliza upya ushahidi huo, ni vizuri kesi hiyo akaifuta ili ifunguliwe nyingine.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika shtaka la kwanza, mshtakiwa anadaiwa katika tarehe tofauti kati ya April 22, 2019, katika jiji la Dar es Salaam, kwa njia ya udanganyifu  alijipatia Sh 315, 079,000 kutoka kwa Ritha Remi, ambaye ni mstaafu kwa malengo ya kufanya biashara, wakati akijua ni uongo.

Shtaka la pili, siku na maeneo hayo, mshtakiwa anadaiwa kughushi namba ya utambulisho ya mlipa kodi( TIN) yenye namba 124-064-218 iliyotolewa Septemba 19, 2016, akionyeshwa kuwa nyaraka hiyo imetolewa na Kamishna wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakati akijua ni uongo.