Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KICHAS kuanzisha stashahada ya juu fani za afya

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC akikabidhi  vyeti kwa wahitimu wa kada mbalimbali  za  afya katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kilimanjaro (KICHAS), kilichopo mjini Moshi  katika mahafali ya saba ya chuo hicho. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Hatua hiyo inalenga kupanua fursa za elimu ya afya na kukidhi ongezeko la mahitaji ya wataalamu wenye umahiri katika utoaji wa huduma bora za afya nchini.

Moshi. Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kilimanjaro (Kichas) kimeandaa mpango wa kuanzisha programu tatu za Stashahada ya Juu katika fani kadhaa.

Fani hizo ni ukunga (Midwifery), uuguzi wa watoto (Paediatric Nursing) na utabibu (Clinical Medicine), hatua inayolenga kuongeza idadi ya wataalamu wa afya wenye ujuzi maalumu nchini.

Akizungumza leo Julai 26,2026 wakati wa mahafali ya saba ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya Kikristo (KCMC), mjini Moshi, Mkuu wa KICHAS, Dk Stephen Kasaizi, amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa chuo kupanua wigo wa mafunzo na kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya sekta ya afya.

Amesema mitaala ya programu hizo tayari imekamilika na inatarajiwa kutoa fursa kwa wahitimu wa fani za afya kuendelea na ngazi za juu za elimu, huku wakiongeza uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dk Kasaizi amesema chuo kinaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia, mafunzo kwa vitendo, utafiti na huduma kwa jamii ili kuhakikisha kinazalisha wataalamu wenye umahiri, weledi na uwezo wa kukabiliana na changamoto za sekta ya afya.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 207 kutoka idara 11 za afya walitunukiwa vyeti na chuo hicho, wakiwemo wanawake 104 na wanaume 103.

Dk Kasaizi, amesema kuanzishwa kwa programu hizo kutatoa fursa kwa wahitimu kujiendeleza kielimu na kuchangia kupunguza upungufu wa wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali ya huduma nchini.

"Katika kuendelea kupanua fursa za elimu chuo kinaendelea na maandalizi ya kuanzisha programu tatu za stashahada ya juu (Higher Diploma) lengo ikiwa  ni kuendelea kuzalisha wataalamu wenye ujuzi, maarifa na maadili ya kazi ambao watasaidia kuboresha huduma za afya nchini," amesema Dk Kasaizi.

Aidha, Dk Kasaizi amesema chuo hicho kimeendelea kuboresha ubora wa ufundishaji, mazingira ya kujifunzia, mafunzo kwa vitendo, utafiti na huduma kwa jamii ili kuzalisha wataalamu wenye umahiri wa kukidhi mahitaji ya sekta ya afya.

Amewakumbusha wahitimu kuwa jamii haitawahukumu kwa vyeti walivyonavyo, bali kwa namna watakavyotekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kwa weledi na maadili.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Profesa Gileard  Masenga amesema sekta ya afya inahitaji wataalamu wenye huruma,  uadilifu, ubunifu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye changamoto, huku wakizingatia maadili ya taaluma zao.

"Elimu mliyopata isiishie kwenye vyeti, bali ionekane katika weledi wenu, maadili yenu na namna mtakavyowahudumia wananchi," alisema.