Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigoma kumuombea Rais Samia siku tano

Mhubiri wa kimataifa wa huduma ya Okoa nafsi zetu (SOS), Adventure kutoka nchi Swiden, Johaness Amrizer (wa pili kushoto) akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Kigoma.

Muktasari:

Kigoma. Mhubiri wa kimataifa wa huduma ya Okoa nafsi zetu (SOS), Adventure kutoka nchi Swiden, Johaness Amrizer anatarajia kufanya sherehe ya kumuombea Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aweze kuongoza nchi kwa hekima na maarifa.

Kigoma. Mhubiri wa kimataifa wa huduma ya Okoa nafsi zetu (SOS), Adventure kutoka nchi Swiden, Johaness Amrizer anatarajia kufanya sherehe ya kumuombea Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aweze kuongoza nchi kwa hekima na maarifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 6, 2021, Amrizer amesema sherehe hizo zitafanyika kwa siku tano kuanzia kesho Jumatano Juni 7 hadi Juni 11 mwaka huu katika kiwanja cha Mwanga Community Center mjini hapa.

Amesema pamoja na neno la Mungu kutolewa pia watakuwa na maombi ya kuombea Serikali Tanzania ya awamu ya sita na kuomba janga la corona ili Mungu aweze kuingilia kati na kuliondoa kabisa.

Alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na janga la corona kwa kutumia njia ya maombi kwa Mwenyezi Mungu na kufanikiwa kulivusha taifa na janga hilo na kwamba maombi hayana budi kuongezwa wakati huu ambapo ugonjwa huo umekuja kwa kasi namna nyingine.


Mwenyekiti wa Makanisa ya Pentekoste mkoani Kigoma, mchungaji Omari Mlenda alisema kuwa pamoja na mahubiri na maombi hayo pia huduma mbalimbali zitatolewa ikiwemo kuwasaidia wagonjwa na wenye mahitaji.

Mchungaji Mlenda alisema kuwa katika siku tano za maombezi na mahubiri hayo watatembelea vituo vya watoto yatima, makazi ya wazee wajioweza na wajane ambako watatoa misaada mbalimbali.

Aliongeza kuwa pia katika siku hizo tano watatembelea shule za msingi na kutoa misaada mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji na wasiojiweza ikiwemo vifaa vya kujifunzia yakiwemo madaftari na kalamu.

Mwimbaji maarufu wa injili nchini, Rose Muhando na Miriam Mauki wanatarajia kutumbuiza katika mahubiri hayo.