Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete atimiza miaka 72, aanza siku kwa mazoezi

Muktasari:

  • Kikwete atimiza miaka 72 leo, aanza siku kwa mazoezi ya kukimbia nyumbani kwake Msoga mkoani Pwani.

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Kikwete ambaye leo anaadhimisha miaka 72 ya kuzaliwa kwake ameanza siku hiyo kwa kufanya mazoezi ya kutembea kilomita tano.

Kikwete ambaye anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa akiwa nyumbani kwake Msoga mkoani Pwani, ameonyesha furaha yake kutimiza umri huo akiwa na afya njema.

“Haya ndiyo maisha yangu ya kila siku asubuhi, tukiamka tunazunguka kuna vilima vikali hapa tunapanda na kushuka,”amesema Kikwete

Akiwa anatembea njiani tukio ambalo limerushwa moja kwa moja na Clouds Media Group, Kikwete ameonekana akizungumza na watu aliokuwa akipishana nao njiani.

Rais huyo mstaafu ameonyesha pia maeneo mbalimbali katika kijiji hicho ambayo yana historia katika maisha yake ikiwemo nyumba aliyozaliwa, shule ya msingi aliyosoma na sehemu alizocheza.