Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Mbowe washinda pingamizi kwa mara ya kwanza

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa ndani ya Mahakama  Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Muktasari:

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imepokea pingamizi la kwanza la kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imepokea pingamizi la kwanza la kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake wameshinda pingamizi hilo baada ya mahakama hiyo kukataa kupokea kielelezo cha kitabu cha kumbukumbu za mahabusu wa kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Mahakama hiyo imesema shahidi ameshindwa kukidhi kigezo kimoja cha namna ambayo kielelezo hicho kimemfikia baada ya kuachana nacho Agosti 5, 2020.