Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinana amwaga sifa kwa Ndugai

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Muktasari:

  • Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana amemsifia Spika wa Bunge Mstaafu Job Ndugai kuhusu maamuzi yake juu ya uchaguzi wa viongozi kwa Mkoa wa Dodoma.

Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema kila uamuzi alioufanya Spika wa Bunge Mstaafu Job Ndugai katika uchaguzi wa viongozi wa Mkoa wa Dodoma ni uamuzi sahihi na haujawahi kutiliwa mashaka.

Kinana ameyasema hayo leo Jumapili Julai 23, 2023 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk Ashatu Kijaji wa kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. 

Kinana amesema wanamheshimu Spika wa Bunge Mstaafu, Job Ndugai na wanatambua mchango wake kwa Taifa na wanathamini uongozi wake wa Bunge la Tanzania. 

Amesema wanatambua kuwa uongozi wake ni hazina kubwa kwa Mkoa wa Dodoma na kwamba amekuwa naye mara nyingi.

“Nimekusikiliza, kila uamuzi ulioufanya katika uchaguzi wa viongozi wa mkoa huu (Dodoma), nimegundua kuwa ni uamuzi sahihi hujawahi kufanya uamuzi ambao umetiliwa mashaka juu ya nani awe nani kwenye nafasi ipi katika mkoa wa Dodoma,”amesema Kinana.

Amesema kauli ya Ndugai nzito katika mkoa huo huwa anatumia busara zake kwa weledi kwa kuwaita wenzake na kusema, “nadhani safari hii twende na huyu safari hii twende na yule tunakushukuru kwa uongozi binafsi.”

Naye Ndugai alimuomba Kinana kufikisha salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa yote yanayofanyika mema kwa ajili ya Tanzania.

 “Tuko naye mguu kwa mguu, hatua kwa hatua safari ni njema na nina hakika kuwa tutafika salama 2025 na hata zaidi ya mwaka 2025,”amesema Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa.