Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwanda cha 'gloves' Idofi kuleta fursa kilimo zao la mpira

Mhandisi wa MSD, Shiwa Mushi akitoa maelezo namna gloves zitakavyotengezwa

Muktasari:

Kuanza kazi kwa kiwanda cha kutengeneza mipira ya mikono Idofi, kutachangia fursa ya ulimaji wa zao la mpira kwa wingi hapa nchini.

Njombe. Kuanza kazi kwa kiwanda cha kutengeneza mipira ya mikono Idofi, Halmashauri  Mji wa Makambako,Mkoani Njombe, kutachangia fursa ya ulimaji wa zao la mpira kwa wingi hapa nchini kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa utomvu wake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Erick Mapunda kwenye ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kiwandani hapo kuona maendeleo ya ujenzi wake ulipofikia.

Kiwanda  hicho ambacho mbali ya kuzalisha glove,pia ndani ya eneo kilipojengwa kuna cha kuzalisha dawa za vidonge na zile za maji pia, kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha gloves 20,000 kwa saa ambapo ni sawa na jozi 10,000 kwa saa.

Akitoa taarifa fupi kwa waandishi hao, Mapunda amesema wakati wakitarajia kuanza uzalishaji Septemba mwaka huu 2022, changamoto kubwa ipo katika upatikanaji wa malighafi ya utomvu aina ya Latex unaotumika kutengenezea gloves hizo na hivyo watalazimika kuagiza nje ya nchi.

"Kutokana na changamoto hizo sasa tutalizimika kuagiza utomvu kutoka nje, lakini ukweli ni kwamba ardhi ya Tanzania inaruhusu upatikanaji wa mpira kwa maana ya ukanda wa Pwani ikiwemo kule Zanzibar," amesema Mapunda.

Pia amebainisha kuwa tayari juhudi mbalimbali zinafanyika ikiwemo mazungumzo na Wizara za kisekta kama kilimo ili kuona watanzania wanahamasishwa kuzalisha zao hili ili waweze kutumia fursa ya malighafi hii katika kiwanda hiko.

Kwa upande wake Mfamasia wa Bohari ya Dawa (MSD), Ezekiel Gadau amesema  mpira unaopatikana hapa nchini ni mpira ghafi ambao hutengeneza matairi na bidhaa zingine wakati wanaouhitaji ni ule ambao umeshachakatwa hadi kufika hatua ya kufaa kutengenezea mipira ya mikono.

"Tumeshafanya mawasiliano na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambao wao ndio wanamiliki mashamba ya mpira yaliyoko Kilombero, Tanga na baadhi ya maeneo ya Pwani, ambao wana uwezo wa kuzalisha mipira kuweza kiifanyia uchakataji huo ili kuweza kupata malighafi hiyo hapahapa  nchini," amesema.

Wakati kuhusu mahitaji, Mhandisi huyo,amesema kwa siku watahitaji tani nne za utovu wa mpira wa mikono,na hivyo kufanya ndani ya miezi mitatu kuwa na mahitaji ya tani 36 ili kuzalisha mipira hiyo ya mikono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa Idofi, namna walivyopekea mradi huo wa viwanda vya dawa akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Yunusi Mhelela, amesema amefarijika na ujio wa kiwanda hiko eneo lake  ambapo wananchi wake wamefaidika kwa kupata ajira na hivyo kupunguza matukio ya uhalifu.

Ofisa Mtendaji Kata ya Idofi, Emmanuel Hauli amesema ujio wa viwanda hiko umepandisha thamani ya ardhi ya eneo hilo na pia Kata yao kutambuliko huku akiomba kuboresha kata hiyo ikiwemo kuwajengea hospitali kwani dawa zitapatiana kirahisi sasa.

Baadhi ya wanannchi wamesema kiwanda kimewanufaisha wananchi hususani wanawake ambao  wamepata kazi na hivyo kusaidia kubadilisha maisha yao ikiwemo kupeleka watoto shule.