Kondomu kutumika kufukuza wanyama wavamiao makazi

Friday May 14 2021
kondumpic

Meatu. Mbinu mpya ya kutumia mabomu ya mkono yanayotengenezwa kwa kondomu ya kiume ili kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu katika makazi ya binadamu, imetajwa kuwa ni bora.

Akiwa kwenye mafunzo ya kukabiliana na wanyama waharibifu yaliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (Tawiri) wilayani Meatu, Meneja wa pori la akiba la Maswa, Jonathan Musiba alisema mbinu ya kutumia mwanga wa tochi na kelele inapokuwa imezoeleka kwa tembo inakuwa haina athari zozote.

Alisema mbinu hiyo inakuwa rafiki na inapotokea mnyama ni mkorofi zaidi inatumika njia mbadala ambayo ni kulipua fataki (Roman candles) Musiba aliwataka wananchi kuzingatia jukumu la kujilinda wenyewe kwa kuepuka kulima mazao yanayopendwa na tembo.

“Wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa hifadhi wajiepushe kulima mahindi pamoja na matikiti maji ambayo tembo wanapendelea zaidi,” alisema Musiba.

Wakielezea adha wanazozipata wakati wanyama, hasa tembo wanapovamia kwenye makazi, vijana waliokuwa kwenye mafunzo hayo walisema:

“Tembo hujifunza kupambana na vikwazo wanavyokutana navyo, akigundua shambani kuna uzio wa pilipili atageuka na kuingia kinyume nyume hivyo kufanya uharibifu, wanapohisi kuna nyuki hawafiki kabisa, hivyo tunalazimika kubuni mbinu mpya kila mara”

Advertisement

Imeandikwa na Samirah Yusuph

Advertisement