Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kortini akidaiwa kujipatia Sh80 milioni kwa njia ya udanganyifu

Mshtakiwa Hassan Omar ( mwenye shati jeusi) anayekabiliwa na shtaka la wizi wa Sh80 milioni, akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Ramdan anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 22, 2026 na Oktoba 21, 2024 eneo la Upanga.

Dar es Salaam. Mhasibu, Hassan  Ramdan (34) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la wizi wa Sh80 milioni, mali ya kampuni ya Preeta Track Company Ltd.

Mshtakiwa amefikishwa Mahakamani hapo, leo Jumatatu Juni 15, 2026 na kusomewa shtaka moja la wizi na wakili wa Serikali, Titus Aron, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Akimsomewa shtaka lake, wakili Aron alidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Julai 22, 2026 na Oktoba 21, 2024 eneo la Upanga, Wilaya la Ilala jini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, mshtakiwa akiwa mfanyakazi wa kampuni hiyo, alijipatia Sh80 milioni mali ya mwajiri wake.

Mshtakiwa baada ya kusomewa kesi hiyo alikana na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hakimu Nyaki alisema shtaka linalomkabili mshtakiwa lina dhamini na hivyo kutoa masharti ya dhamana.

Mshtakiwa ametakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria.

Vilevile mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh40 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo kurudishwa rumande hadi Juni 29, 2026 kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huohuo, mfanyabiashara na raia wa Kenya, Victor Okoye (51) amefikishwa katika Mahakama hiyo kujibu shtaka moja la kukutwa na mali inayodaiwa kuwa ya wizi.

Okoye amesomewa shtaka lake na wakili wa Serikali Titus Aron, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Wakili Aron alidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 11, 2026 eneo la Sinza.

Inadaiwa siku na eneo hilo, mshtakiwa alikutwa na gari aina ya Toyota Land Cruise Prado, linalodaiwa kuwa la wizi.

Mshtakiwa amekana shtaka na kesi yake imeahirishwa hadi Juni 29, 2026 na amerudishwa rumande.