Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndugu kortini wakidaiwa kutakatisha Sh310 milioni

Mshtakiwa John Kashiha  (40) na mdogo wake, Lightness Kashiha(32) wakiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, baada ya kusomewa kesi ya uhujumu uchumi. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • John na Lightness wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kulisababishia hasara shirika na kutakatisha kiasi hicho cha fedha tukio wanalodaiwa kutenda, Mei 18, 2023 katika Jiji la Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Wakurugenzi wawili wa Kampuni ya Tuzo Business Group of Company Limited, John Kashiha (40) na Lightness Kashiha (32) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la wizi wa Sh310 milioni, mali ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).

John mkazi wa Kinondoni na mdogo wake Lightness mkazi wa Madale, wanadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka TPC, kwa madai wangewapelekea magari tisa, wakati wakijua ni uongo.

Washtakiwa hao, wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne, Juni 9, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 12688 ya mwaka 2026 na wakili wa Serikali Titus Aron, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Hata hivyo, kabla ya kusomewa mashtaka yao, hakimu Nyaki aliwaeleza washtakiwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo isipokuwa kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mshtakiwa John Kashiha  (40) na mdogo wake, Lightness Kashiha(32) wakiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, baada ya kusomewa kesi ya uhujumu uchumi. Picha na Hadija Jumanne

Pia, shtaka la kutakatisha fedha halina dhamana kwa washtakiwa hao, hivyo watapelekwa rumande.

Hakimu Nyaki, baada ya kutoa maelezo hayo, wakili Aron aliwasomea mashtaka yao.

Alidai shtaka la kwanza ni kulisababishia hasara Shirika la Posta Tanzania, ambapo washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Mei 18, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa ni wakala wa TPC, walilisababishia hasara ya Sh310 milioni shirika hilo.

Shtaka la pili, tarehe na eneo hilo washtakiwa kwa njia ya udanganyifu walijipatia Sh310 milioni kutoka TPC kwa madai kuwa wangelipeleka shirika hilo magari tisa, huku wakijua kuwa ni uongo.

Mshtakiwa John Kashiha  (40) na mdogo wake, Lightness Kashiha(32) wakiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, baada ya kusomewa kesi ya uhujumu uchumi. Picha na Hadija Jumanne

Iliendelea kudaiwa mahakamani hapo kuwa shtaka la tatu ni kutakatisha fedha  linalowahusu washtakiwa wote.

Wakili Aron alidai tarehe na eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja walijipatia Sh310 milioni kutoka TPC, wakati wakijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Beda aliahirisha kesi hadi Juni 19, 2026 kwa kutajwa.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.