Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kumuua mpenziwe Dar kuendelea kusota rumande hadi Juni 23

Mshtakiwa Rehema Hassan (katika) anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya muongozaji na Msimamizi wa sauti za filamu nchini, Athuman Nyanza, akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi, siku alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Rehema anadaiwa kumuua mwongoza filamu nchini, Athuman Nyanza tukio analodaiwa kulitenda Februari 10, 2026 eneo la Mwapemba, Kigamboni.

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara, Rehema Hassan (42), umedai bado unaendelea na uchunguzi.

Kwa tafsiri hiyo, Rehema ambaye ni mkazi wa Kigamboni Mwapemba, ataendelea kusalia mahabusu hadi Juni 23, 2026 kesi hiyo itakapotajwa kwa njia ya mtandao.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokukamilika.Rehema anadaiwa kumuua mwongozaji na msimamizi wa sauti za filamu nchini, Athuman Nyanza.

Leo Jumanne, Juni 9, 2026 Wakili wa Serikali, Erick Mabagala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa njia ya video huku mshtakiwa akiwa mahabusu.

"Mshtakiwa hajaletwa mahakamani hapa na upelelezi wake bado unaendelea na uchunguzi, kwa sababu hii tunaomba Mahakama itupangie tarehe nyingine," amesema Wakili Mabagala.

Mbagala ametoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, anayesikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mwankuga, amekubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 23, 2026.

Mshtakiwa Rehema Hassan (katika) anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya muongozaji na Msimamizi wa sauti za filamu nchini, Athuman Nyanza, akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi, siku alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Hadija Jumanne


Kesi ya msingi

Rehema anadaiwa Februari 10, 2026 eneo la Mwapemba lililopo Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, ulimuua Athuman Nyanza.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kinyume na kifungu 196 na kifungu 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa alifikishwa Mahakamani hapo Aprili 29, 2026 na kusomewa shtaka hilo.

Hata hivyo, kesi ya mauaji ni miongoni mwa mashtaka ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria na ndio sababu ya Rehema kuendelea kusalia rumande.