Kortini akidaiwa kumwingilia ng'ombe

Muktasari:

  • Watu wawili wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, wamepandishwa kizimbani kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Wilaya ya Siha, wakikabiliwa makosa mawili tofauti, likiwemo a la kumwingilia ng'ombe, na la ubakaji.

Siha. Mkazi wa Kijiji cha Ngaron, wilayani hapa, Kelvin kileo (28) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Siha, kwa kosa la kumwingilia ng'ombe.

Akisoma mashitaka hayo Januari 22, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Jasmini Abduli, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, David Chisimba ameieleza Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 13, mwaka huu kwa kumwingilia ng'ombe wa jirani.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo, na baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana, alirudishwa rumande hadi Februari 8, mwaka huu ambapo shitaka hilo litakapokuja tena mahakamani hapo.

Wakati hou huo, Mkazi mwingine wa Kijiji cha Sanya juu, wilayani humo, Issa Chado (53) amefikishwa mahakamani hapo, kwa kosa la kubaka watoto wawili wa kike wenye umri wa miaka 6 na kuwasababishia maumivu makali.

Mwendesha mashitaka huyo wa Serikali, ameieleza mahakama hiyo kuwa, mshitakiwa huyo kwa nyakati tofauti tofauti alikuwa akiwaingilia watoto hao, huku akifahamu kufanya hivyo ni kosa.

Jana Januari 22, 2024 Chisimba ameieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo, alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na 131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ambayo ilifanyiwa marejeo mwaka 2022.

Hata hivyo mshitakiwa huyo, alikana mashitaka na baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana, pia alipelekwa rumande hadi Februari Mosi, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa mara ya pili.