Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu kortini akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake

Muktasari:

Mwalimu wa shule ya sekondari ya kutwa Nyang'homango wilayani hapa mkoani Mwanza, Nicholaus Emmanuel (40) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi kwa tuhuma ya kumpa ujauzito mwanafunzi wake.

Misungwi. Mwalimu wa shule ya sekondari ya kutwa Nyang'homango wilayani hapa mkoani Mwanza, Nicholaus Emmanuel (40) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi kwa tuhuma ya kumpa ujauzito mwanafunzi wake.

Akimsomea mashtaka yake katika shauri namba 96/2023 ya makosa ya jinai mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo, Amani Shao, mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa Polisi, Ramsoney Salehe amedai mtuhumiwa alifanya mapenzi na mwanafunzi huyo kwa tarehe tofauti Juni mwaka huu.

Ameieleza Mahakama kwamba kabla mtuhumiwa hajabadilishwa kituo cha kazi alikuwa sekondari ya Nkalate, alifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Nkalete mwenye umri wa miaka 18 na kumpatia ujauzito.

Amedai kwamba kufanya mapenzi na kumpatia ujauzito mwanafunzi huyo  ni kinyume cha sheria ya elimu kifungu cha 60 (A) kifungu kidogo (4) sura 353 kama kilivyorejelewa na sheria namba mbili ya mwaka 2016.

Hakimu Shao alimuuliza mtuhumiwa kuhusiana na tuhuma hiyo kama ni kweli mtuhumiwa alikataa kuwa sio kweli na Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 6 mwaka huu, mtuhumiwa atakapofika mahakamani kusomewa hoja za awali na upande wa mashitaka uko tayari kuanza kusikiliza ushahidi wake.