Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 30 jela kwa ubakaji, unyang'anyi wa kutumia silaha

Mshtakiwa Godi Kisungura akipanda gari la Polisi baada ya  Mahakama ya Wilaya Mufindi kutoa hukumu yake ya miaka 30 jela ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba kuzitumikia.Picha na Mary Sanyiwa

Mufindi. Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemuhukumu kutumia kifungo cha miaka (30) Jela God Kisungura (30) Mkazi wa kijiji cha Ipilimo, Kata ya Mtambula, Tarafa ya Kasanga baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ikiwemo la unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na kumbaka mwanamke mwenye umri (62)

Shauli hilo namba 15, 2023 ambalo hukumu yake imetolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa Sekela Kyungu.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema kuwa Kisungura ametenda kosa hilo December 15, 2022 saa 1:00 usiku, kijiji hapo akiwa nyumbani kwa muathirika wa tukio hilo, akidai kwamba alifika kumuandikisha jina ili apate mbolea za ruzuku.

"Ili kufanikisha azma yake, Kisungura alimkaba muathirika na kumwambia ampe pesa ndipo akapewa Sh30, 000; hata hivyo aliomba aongezewe pesa, ndipo akaambiwa ziko chumbani ambako waliongozana na akapewa Sh300, 000; na hivyo kufanikiwa kupata jumla ya Sh330, 000,” amesema na kuongeza;

Baada ya kupewa fedha hizo, Kisungura anadaiwa kumbaka na alipomaliza haja zake, alimpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na mikononi, hali iliyomsababisha mama huyo kuvunjika kidole gumba,” amesema hakimu huyo.

Hakimu Kyungu amefafanua kuwa hukumu aliyotoa ni kwa kwa makosa mawili ambayo ni lile la la unyang'anyi wa kutumia silaha, ambalo ni kinyume na kifungu namba 287A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la Mwaka 2022 pamoja; na la pili ni la ubakaji ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na kifungu 131(1) cha sheria za kanunu ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022.

"Mshtakiwa amehukumiwa kwa shtaka la kwanza na shtaka la pili kifungo cha miaka 30 jela, kwa mujibu wa kufungu namba 131(1) la Sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 rejeo la mwaka 2022 kwa kosa la ubakaji na kifungu namba 287A kosa la unyang'anyi kwa kutumia silaha, adhabu zote zitaenda sambamba kutumikia kifungo hicho,” amesema Kyungu.

Kyungu amesema kuwa Mahakama imetoa adhabu hiyo ya kifungo cha Miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa mshtakiwa pamoja na jamii wenye tabia kama hiyo.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakali wa Serikali, Ahmed Magenda, amesema kuwa hana kumbukumbu yote ya makosa mengine ya jinai kwa mKisungura, huku akiomba mahakama itoke adhabu kali ili jamii iweze kujifunza kutokana na makosa hayo.

Alipopewa nafasi ya kujitetea ya kutoa ombi lake kabla ya hukumu, Kisungura aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa makosa hayo kwani ana familia ambayo itaishi katika mazingira magumu mara baada hukumu hiyo.

Hata hivyo, mahakama ilitupilia mbali ombi hilo.