Kundi jingine la nzige laingia Tanzania

Kundi jingine la nzige laingia Tanzania

Muktasari:

  • Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amesema wakati serikali ikipambana kuwaangamiza nzige wa jangwani  walioingia nchini Februari mwaka huu limeingia kundi jingine jipya likitokea nchi ya Kenya.

Moshi. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amesema wakati serikali ikipambana kuwaangamiza nzige wa jangwani  walioingia nchini Februari mwaka huu limeingia kundi jingine jipya likitokea nchi ya Kenya.

Profesa Mkenda ameyasema hayo leo, Machi mosi mwaka huu wakati akizungumza na vyombo vya habari mjini Moshi juu ya tathmini ya mwenendo wa kupambana na nzige hao.


Kundi jingine la nzige laingia Tanzania


Aidha amesema serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha nzige hao wanaangamizwa tayari na ndege ya Shirika la Kupambana na Nzige wekundu kutoka Zambia ipo katika wilaya ya Longido kupambana na nzige hao.

"Kundi jipya la nzige limeingia nchini likitokea Kenya na liko Longido ambako kuna ndege kutoka Shirika la Kupambana na Nzige wekundu tayari kupambana na nzige hawa.

"Tumepata taarifa kuna kundi jingine limetokea Machakos nchini Kenya na upepo unaweza kuwapeleka upande wa Kajiado huko Kenya pia, sasa nzige hao wanaweza kuja Tanzania lakini tunawasiliana na Kenya ili wawahi huko,"amesema Profesa Mkenda.