Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LIVE: Malimbikizo ya mishahara, posho zawakuna wafanyakazi

Muktasari:

Wakati wafanyakazi wakiadhimisha siku yao leo Jumatatu Mei Mosi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa ametaja baadhi ya mambo ambayo wafanyakazi wanaishukuru Serikali kuwa ni pamoja na kushughulikiwa kwa kero za muda mrefu za wafanyakazi.


Dar es Salaam. Wakati wafanyakazi wakiadhimisha siku yao leo Jumatatu Mei Mosi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa ametaja baadhi ya mambo ambayo wafanyakazi wanaishukuru Serikali kuwa ni pamoja na kushughulikiwa kwa kero za muda mrefu za wafanyakazi.

Ametaja kero hizo kuwa ni pamoja na kushughulikiwa kwa malimbikizo ya madeni ambayo wafanyakazi waliidai Serikali kwa muda mrefu, nyongeza ya mishahara na posho za safari.

Julai Mosi 2022 Rais Samia Suluhu Hassan alitoa kibali cha kurekebisha posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa watumishi wa umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum kwa watumishi hao nchini kutoka Sh120,000 hadi Sh250,000 kwa kiwango cha juu na Sh80,000 hadi Sh100,000 kwa kiwango cha chini.

LIVE: Rais Samia ashiriki maadhimisho ya Mei Mosi Morogoro

Mwasa ameyasema hayo leo mkoani Morogoro katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa (Mei Mosi) ambazo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tumeona maboresho maeneo mengi ambapo umeongeza ajira kwenye sekta za elimu, afya, maji na umeme kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta hiyo.

“Wafanyakazi wa sekta ya umma tunakupongeza kwa namna unavyotujali, tangu umeingia madarakani wametatuliwa sekta zao nyingi zilizokuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu ikiwemo posho za safari na kulipwa malimbikizo ya madeni yao,” amesema Mwasa.

Aidha amesema kwa Mkoa wa Morogoro jumla ya wafanyakazi 1,708 waliostahili wamepandishwa vyeo,  2,030 waliajiriwa kupitia ajira mpya na sasa Rais ametangaza ajira mpya 3,861.

“Mkoa tutaongeza ajira katika sekta binafsi, tumejipanga kuweka ranchi mpya ya kisasa kwa ajili ya ajira kwa vijana na kupitia haya tumetenga fedha za kujenga karakana za vijana lengo ni kuongeza ajira za vijana, tumepanga kujenga soko kubwa kwa kundi hilo na wanawake mkoani Mogorogo,” amesema.

Aidha amelishukuru Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kuamua kufanya shughuli hiyo Morogoro. “Tunashkuru wanamichezo wote mlioshiriki katika juma la wafanyakazi lililofanyika hapa, mkoa umeinuka kimapato,” amesema Mwasa.