Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maadhimisho ya Kiswahili Duniani  kufanyika Julai nchini Burundi

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA), Dk Caroline Asiimwe, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar.

Muktasari:

  • Nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakutana Bujumbura, Burundi katika kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani pamoja na Kongamano la Kakama.

Zanzibar. Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kakama) imetangaza maadhimisho ya Siku Kiswahili kuwakutanisha wananchi kutoka mataifa manane ya Afrika Mashariki mjini Bujumbura, Burundi.

Akizungumza leo Juni 19,2026 na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili (Kakama), Dk Caroline Asiimwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Julai 5-7, 2026.

Amesema maadhimisho ya Kiswahili yatatanguliwa na Kongamano la Tatu ka Kakama na kufuatiwa na Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7.

Amesema maadhimisho ya kongamano la Kakama yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili na kutoa fursa kwa kila nchi wanachama.

Amesisitiza kwamba maadhimisho hayo yamewezesha wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kunufaika na fursa mbalimbali kupitia Kiswahili.

Aidha lugha ya Kiswahili imetajwa kufikia hadhi ya kimataifa kiwango cha kuwezesha kuwa na mchango wa maendeleo katika nchi wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema lugha ya Kiswahili inaweza kumwezesha mwekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika nchi husika kutokana na kutumika na takribani nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo lugha ya Kiswahili inatambulika rasmi na kuzungumzwa.

Dk Asiimwe amesema lugha ya Kiswahili inamwezesha hata mjasiriamali na mfanyabiashara aliyepo kijijini kuamua kuchagua lugha atakayo kupitia akili unde ili kumwezesha kuwasiliana kikamilifu.

Amesema kutokana na maendeleo ya teknolojia, yamewasukuma katika maadhimisho ya Kiswahili mwaka huu kubeba mjadala wa akili unde na wingi lugha.